Unachoweza kufanya kujikinga na maambukizi mapya ya corona

October 7, 2022 8:44 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Waliowahi kupata corona na wakapona wapo kwenye hatari ya kupata tena virusi hivyo.
  • Watu ambao hawajapata chanjo wapo kwenye hatari zaidi ya maambukizi mapya.

Dar es Salaam. Wakati dunia ikiendelea na mapambano dhidi ya janga la uviko-19, kumeibuka hofu miongoni mwa watu juu ya uwezekano wa kupata tena virusi hivi na kurudi kwenye maradhi na vifo vinavyoendelea kumaliza maisha ya watu duniani.

Kama wewe ni mmoja wa watu wenye hofu ya kuukwaa kwa mara ya pili ugonjwa huu, nikutoe shaka kwamba kuna njia ambazo unaweza kuzitumia kujiepusha na maambukizi hayo kwa mara nyingine.

Kwa mujibu wa Kituo cha Kinga na Udhibiti wa Magonjwa (CDC), mtu aliyewahi kupata ugonjwa  wa Corona na akapona  yupo kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa tena virusi hivyo kwa mara nginine.

“Virusi vinabadilika kila wakati, ikiwemo  virusi vinavyosababisha Uviko-19. Mabadiliko haya yanaweza kusababisha aina mpya za virusi ambazo zinaweza kuongeza hatari ya maambukizi mapya,” inasema taarifa ya CDC iliyotolewa 9 Septemba, 2022

Ripoti ya utafiti  wa kituo hicho uliotolewa 21 Agosti, 2021  iliyopewa jina la ‘kupunguza hatari ya maambukizi ya uviko 19 kwenye mji wa Kentucky nchini Marekani kwa mwezi Mei na Juni 2021” umeonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa mtu kuambukizwa tena uviko-19 muda mfupi baada ya kupon ugonjwa huo.

Hata hivyo, hatari hiyo inaweza kuwakabili zaidi watu ambao bado hawapata chanjo ya Uviko-19.


Soma zaidi:


Unawezaje kujikinga na Uviko-19 usikupate tena?

Zipo njia nyingi za kujikinga na maambukizi ya uvikiko-19 kwa mara ya pili, japo njia hizi zinafanana na zile za kujikinga na maambukizi mapya kama zinavyoainishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Hatua ya kwanza unayoweza kuchukua kukabiliana na maambukizi ya mara ya pili ni kupata chanjo kwa wakati sahihi.

Hakikisha unanawa mikono kila mara kwa kutumia sabuni na maji tiririka kwa angalau sekunde 20, ama tumia kitakasa mikono. Kwa kufanya hivyo utakuwa una jikinga na Uviko-19.

Vaa barakoa unapokua sehemu zenye watu wengi kama vile sokoni ama kwenye usafiri wa umma. Hii ni muhimu hasa katika maeneo yenye maambukizi makubwa ya ugonjwa huo.

Funika mdomo wako na pua kwa kutumia kiwiko ama tishu unapokohoa ama kupiga chafya. Tupa tishu sehemu salama baada ya kuitumia.

Kumbuka kukaa umbali kati yako na watu wengine kadiri inavyowezekana. Hii inamaanisha kukaa umbali wa mita 1 kati yako na watu wengine, epuka mikusanyiko na maeneo yenye watu wengi

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV