The Suicide Squad: Filamu ya waovu tumaini la dunia

July 30, 2021 2:39 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu inayoeleza kisa cha waovu kupewa kazi ya kuikomboa dunia.
  • Waliopewa kazi hiyo wanatambua kuwa “mission” yao, ni njia kuelekea kifo.

 Kusikiliza uchambuzi wa filamu hii, sikiliza hapa                       

                                       


Dar es Salaam. Pale Superman anapokufa, ulimwengu unabaki bila shujaa wa kumtegemea. Lakini Afisa wa Intelijensia nchini Marekani, Amanda Waller anaishawishi Serikali kuridhia kutengenezwa kwa kikundi cha magaidi walioshindikana.

Kikundi hicho cha wafungwa kinapewa kazi moja ya kuikomboa dunia kwa ahadi ya kuwapunguzia miaka 10 kwenye vifungo vyao. Kikundi hicho ni The Suicide Squad.

Kwa muda mrefu Marekani imekuwa ikimtegemea shujaa Superman kuikomboa na matatizo ya kila siku. 

Ugaidi, majambazi, wizi wa hapa na pale na hata dhidi ya viumbe wa ajabu wanaokuja duniani kutoka sayari zingine ni miongoni mwa matatizo yanayoitesa nchi hiyo.

Superman ni kama polisi ambaye humpatia kila mtenda maovu haki yake. 

Kwa sasa jambo kubwa zaidi linatarajiwa kuikumba dunia lakini Superman aliyetegemewa kuikomboa Marekani amefariki. Yote ilianza baada ya Bloodshot kukatisha maisha ya shujaa huyo. 

Pale dunia inapokosa tumaini la shujaa, waharamia wanabaki tumaini pekee. Picha| joblo.com 

Kufariki kwake ni tangazo la kuwa, hakuna mtu wa kuwatetea wanyonge na hivyo dunia inabakia uwanja wa michezo kwa watenda maovu wote akiwemo Dk June Moone na mradi wake wa “The star project” ambao bila shaka ni tishio kwa maisha ya wanadamu.

Kulizuia hilo, kundi mkakati inabidi litengenezwe na wanaotengenezakundi hilo siyo wengine bali magaidi walioshindikana, waliotumia maisha yao yote, kupambana na mashujaa akiwemo Superman.

Kukuelewesha kuhusu magaidi hao, hawa ni wale watu ambao hawapendi mashujaa. Yaani kazi yao kubwa duniani ni kuhakikisha mashujaa hawafanyi kazi zao. 

Naweza kukupa mfano wa Superman na Bloodshot, Spiderman na Mysterial na wengine orodha inaendelea.

Ikiwa kila mtu akiwa na kipawa chake, kikundi hiki kinaundwa na magaidi kama Deadshot, Dr Harleen, Ric Flag, Captain Boomerang, El Diablo, Killer Croc, Katana na wengine wengi.

Suicide squad kuikomboa dunia

Kumbuka kuwa watu hawa sio watu ambao jamii inawakubali. Ni watu ambao kwa maisha yao yote kwa namna fulani, wamehusika katika kudondosha chozi kwa wananchi. Uwezekano wa watu kuwapa ushirikiano ni mdogo au haupo kabisa.

Hata hivyo, bado kazi yao inaendelea. 

Pale wanapoanza safari ya kumtafuta Dk Moone huko Midway City, helikopta yao inalipuliwa na wanadondokea pasikojulikana.

Kwa kukosa njia nyingine ya kufika sehemu wanapotakiwa kwenda, inabidi watembee.

                        

Katika safari hiyo wanagundua mambo mengi ambayo yanawaacha njia panda ikiwemo mahusiano kati ya Flag ambaye anahusika katika kuwapatia misheni yao na Dk Moone ambaye wanamtafuta. 

Cha ajabu zaidi, hata Waller, naye kumbe hakuwapatia taarifa zote za kuhusika na Dk Moone kwa namna fulani.

Watafanyaje ikiwa hawawezi kukimbia wala kujitoa kwenye misheni hiyo?

Ni maamuzi ya Suicide squad kupembua mbivu na mbichi na kama kweli bado ipo haja ya kuendelea na safari yao.

Ikiwa ni nafasi ya waovu hao kuonyesha ulimwengu kuwa wanaweza kufanya mambo mazuri wanapoamua, ulizo ni kama wapo tayari kufanya hivyo.

Usaliti, ukweli uliofichwa, visasi na historia inayowawinda wahusika ni sehemu ya filamu hii iliyojaa nyota wa filamu akiwemo Viola Davis, John Cena, Idris Elba, Margott Robbie, Sylvester Stallone na Pete Davidson.

Pale Starfish anapokuwa sio mdogo tena, dunia inategemea waharamia kuikomboa. Tazama filamu hii ya “The Suicide Squad” kupitia kumbi za kuangalia sinema na usisite kutupatia mrejesho wako kupitia kurasa za mitandao ya kijamii.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW