The Archenemy: Filamu inayokupa sababu za kutokumdaharau mtu usiyemjua

February 5, 2021 12:31 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Filamu inamhusu kijana mwenye ndoto za kuwa mwandishi wa habari za uhalifu anayekutana na chokoraa Max Fist.
  • Max anasema yeye siyo wa dunia hii na uwepo wake duniani ndio unamfanya asiwe na nguvu zake za maajabu.
  • Licha ya kuwa hana nguvu, analazimika kupambana vilivyo kuhakikisha usalama wa rafiki zake dhidi ya magwiji wa dawa za kulevya.

Dar es salaam. Nakumbuka wakati tulivyokuwa watoto, tulifundishwa kutokudharau mtu ambaye hatumjui kwani huenda akakusaidia mbeleni.

Tulifundishwa kusalimia watu pale tunapokuwa ugenini kwani watu hao huenda wakawa msaada pale utakapokuwa umepotea na unahitaji kuelekezwa.

Kwa bwana mdogo Hamster (Skylan Brooks), huenda mafundisho hayo yalimuingia vilivyo kwani anapokutana na Max Fist (Joe Manganiello), bado anamheshimu licha ya kuwa kwa jamii ya Kitanzania, Max angelitambulika kama chokoraa.

Kisa hichi kiko kwenye filamu ya The Archenemy. 

Imani ya Hamster juu ya Max ni kubwa kiasi cha kutokutaka kusikia la kuambiwa juu yake kwani anaamini maneno ambayo Max anayasema kuhusiana na nguvu zake za maajabu. 

Ikiwa malengo ya kijana huyo ni kuwa mwandishi wa habari za uharifu, anachukua  nafasi ya kuwa msaidizi kwa Max ambaye anadai amepoteza nguvu zake.

Kwa wengine, ni vichekesho na wanamchukulia Max kama mtu asiyejielewa na aliyepoteza dira ya maisha yake.

Hata hivyo, anachodai Max ni kuwa yeye siyo mtu wa dunia hii bali ni mwana mpotevu aliyetengwa mbali na dunia yake na uwepo wake duniani unaathiri nguvu za maajabu ama waweza kuziita “super powers” alizokuwa nazo.

“Nilikua nikikaa katika majengo marefu zaidi duniani kwetu na ninaangalia chini kama Mungu,” ni Max akielezea maisha yake ya awali kabla ya kuwa mlevi.


Soma zaidi:


Anachokidai Max ni kuwa, duniani kwake pombe kidogo tu ingemtosha lakini hata pombe kali zaidi katika dunia ya Hamster, haijafanya lolote kwake.

Filamu hii inamuhusu Hamster na dada yake Indigo (Zolee Griggs) ambao ni yatima wanaopigana kujinasua dhidi ya mtandao wa wauzaji wa madawa ya kulevya na sukari inakolea zaidi wanapokutana na Max ambaye anajitoa mhanga kuhakikisha usalama wa rafiki zake wapya.

Fuatilia filamu hii kupitia skrini za sinema nchini na katika baadhi ya mitandao itakayokuhitaji kuwa na GB za kutosha.

Pia unaweza kuisikiliza habari hii kupitia Soundcloud kwa kubonyeza alama ya “play”

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV