“The Last Thing He Wanted”: Filamu inayokusubiri wikiendi hii

October 2, 2020 12:56 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu inayomhusu mwandishi wa habari anayejulikana kama Ellie.
  • Wakati akifanya habari za kiuchunguzi anajikuta akiangukia chini ya macho ya wasiopenda kufuatiliwa.
  • Kufiwa na baba yake, kunusurika kufa, hofu juu ya mtoto na familia yake ni sehemu ya visa vya filamu hii.

Dar es Salaam. Elena McMahon ni mwandishi wa habari za uchunguzi anafanya uchunguzi juu ya biashara ya silaha inayofanyika nchini Marekani.

Wakati akichimba habari hiyo, anajikuta amejivika visivyovalika baada ya Richard McMahon ambaye ni baba yake kumhusisha na biashara ya silaha wakati akiwa kwenye siku za mwisho za maisha yake.

Ufukunyuku wa mwanadada huyo unamfanya adondokee kwenye rada za watu wasiopenda “wambea” kama yeye.

Familia iliyovunjika, baba anayeaga dunia, mtoto anayemlilia na kazi zinazomuelemea ni sehemu ya kimbembe kinachomsibu mwanadada huyu ambaye ni mwandishi mashuhuli wa habari.


Soma zaidi


Ataweza kuishi endapo kila hatua yake iko chini ya uangalizi? Fuatilia filamu ya The Last Thing He Wanted katika mtandao wa Netflix ambapo utakutana na waigizaji maarufu wakiwemo Anne Hathaway, Willem Dafoe na Rosie Perez wakikungoja kukonga moyo wako.

Kama filamu siyo fungu lako, wikiendi hii inaweza kuwa njema kwako kama utaamua kutoka mtoko na kupumzika nyumbani na familia.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV