The Markman: Filamu kwa ajili ya wikiendi yako

January 30, 2021 8:12 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Inamhusu mwanajeshi mstaafu ambaye anakiuka maadili kwa ajili ya kuokoa maisha. 
  • Kitendo hicho kinamponza kwani ameweka pua yake mahali isipostahili.
  • Baada ya kuokoa maisha ya mtoto Miguel, usalama wake unabaki katika mikono yake.

Dar es Salaam. Kila kitu huwa sawa hadi pale “utakapoiweka pua yako mahala isipostahili” maneno hayo ni tafsiri ya nahau ya Kiingereza inayosema “sticking your nose where it doesnt belong” ambayo kwa maana nyingine ni kuingilia yasiyokuhusu.

Jim Hanson ni mwanajeshi mstaafu ambaye makazi yake yapo mpakani mwa Mexico na Arizona. Anachokifanya baada ya kustaafu, ni kutoa taarifa za watu wanaovuka mpaka huo kwa njia zisizo za halali. 

Siku moja wakati akiwa kwenye zamu yake ya ulinzi, alikutana na mwanamama Rosa akiwa na mwanaye Miguel ambao walikuwa wakikimbizwa na genge la majambazi waliokuwa wakitaka kuyadai maisha ya wawili hao. 

Hanson, hakutakiwa kuwaruhusu Rosa na mwanaye kuvuka mpaka huo lakini kwa kuingiwa na huruma, alianzisha majibizano na majambazi hao na kuwatorosha Rosa na Miguel. 

Huruma yake, haigusi mioyo ya majambazi hao wanaoongozwa na Maurico.

Bahati mbaya ni kuwa, katika mashambulizi hayo, maisha ya Rosa yanafika tamati baada ya kipigwa risasi iliyoyadai maisha yake. Kwa Hanson, hana budi bali kuendelea kutafuta usalama wa kijana Miguel.


Soma zaidi;


Wanasema ukianzisha ugomvi wa mawe, hakikisha nyumba yako siyo ya vioo. Kwa Hanson ambaye ameanzisha ugomvi na Maurico, huenda akawa amefanya maamuzi mabaya ya maisha yake.

Mkasa huu unaendelea kupitia skrini za Century Cinemax huku kitendawili cha usalama wa maisha ya Miguel kikijibiwa kwa gharama ya Sh10,000 tu.

Unapenda simulizi za kusisimua zilizojaa “mkono” wa kutosha? fuatilia filamu hii ya The “Marksman” kama burudani ya wikiendi yako inayomleta mpambanaji Liam Neeson karibu na wewe.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
NISHATI

NISHATI

Nukta TV

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Nukta TV

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Nukta TV