Tanapa yakamilisha ukarabati wa barabara hifadhi ya Serengeti

March 10, 2024 12:24 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Yasema ubovu wa barabara ulikwamisha baadhi ya shughuli za utalii.
  • Sasa barabara zitajengwa kwa lami ngumu.

Dar es Salaam. Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) limesema limekamilisha ukarabati wa awali wa  barabara na maeneo  yalioathiriwa na mvua za El Nino katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambazo zilizuia baadhi ya shughuli za utalii kufanyika katika hifadhi hiyo.

Itakumbukwa kuwa miezi michache iliyopita Tanzania ilishuhudia uharibifu mkubwa wa nyumba, madaraja na barabara kutoka na mvua za El Nino  zilizoanza kunyesha mwezi Oktoba mwaka huu.

Kutokana na mvua hizo, takribani kilomita 2,407 za barabara za udongo na kilomita 769 za changarawe katika hifadhi ya Serengeti zilijaa maji na kuzuia baadhi ya shughuli za kitalii kuendelea ikiwemo usafirishaji.


Soma zaidi:Waziri Kairuki azindua kamati ya kitaifa ya kuongoa shoroba


Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi, aliyekuwa akizungumza na wanahabari leo Machi 10, 2024 jijini Dodoma  amesema kwa sasa barabara hizo za hifadhi ya Serengeti ambayo ni miongoni mwa hifadhi kubwa nchini zinapitika na watalii wataendelea kupatiwa huduma kama iliyokuwa awali.

“Tanapa katika hatua za awali imekamilisha matengenezo na sasa barabara hizo zinapitika na watalii wanaendelea kupata huduma zinazostahili,” amesema Matinyi.

Huenda marekebisho hayo katika hifadhi ya Serengeti yakapaisha zaidi idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi hiyo ambapo hadi kufikia mwezi Februari mwaka huu watalii milioni 1.4 walitembelea hifadhi hiyo.

Idadi hiyo ya watalii waliongia nchini ni asilimia 0.04 zaidi ya lengo lililowekwa na Serikali la kupokea watalii milioni 1.3 hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu.

Aidha, Matinyi amesema kwa sasa Tanapa  inatafuta njia mbadala wa kuhifadhi barbara hizo ikiwemo kuzijenga kwa lami ngumu na zege ili ziweze kustahimili mvua na mabadiliko ya hali ya hewa yanayoweza kutokea pia kutokana na kuadimika kwa malighafi ya changarawe.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV