Maeneo 10 kukuza uchumi wa Tanzania 2024-25

June 13, 2024 9:21 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kukuza uzalishaji katika sekta ya kilimo na viwanda

Dar es Salaam. Serikali imesema ili kufikia vipaumbe vitano vya bajeti ya 2024/25 ikiwemo ukuaji wa uchumi jumuishi, itaweka msisitizo katika masuala 10 ikiwemo kuendelea kuwekeza katika kukuza uzalishaji katika sekta ya kilimo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amewaeleza wabunge jijini Dodoma leo Juni 13, 2024 kuwa uzalishaji huo wa bidhaa za kilimo utasaidia kulisha viwanda vya ndani na nje ya nchi hivyo kukuza uchumi.

“Kama tunavyofahamu, uchumi wa viwanda tunaojaribu kuujenga malighafi zake nyingi zinategemea kilimo. Aidha, katika kipindi cha muda mfupi na muda wa kati, Watanzania wengi wataendelea kuajiriwa na kujiajiri katika sekta ya kilimo, hivyo, hatuwezi kuzungumzia mapinduzi ya viwanda bila kuzungumzia mapinduzi ya kilimo,” amesema Prof Kitila.

Meneo mengine ni uwekezaji katika viwanda ili kuchochea uzalishaji wa bidhaa muhimu na kuimarisha biashara na uwekezaji mdogo na wa kati pamoja na kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za Taifa. zikiwemo gesi, madini, misitu, bandari na maziwa.

“Serikali itahakikisha kuwa nchi yetu inapunguza na hatimaye kuzuia kabisa kusafirisha kama malighafi rasilimali zinazovunwa kutoka katika ardhi, misitu na maji ya Tanzania na  kuweka mazingira ya kisera na kisheria yatakayohakikisha kuwa rasilimali hizi zinachakatwa na kuongezewa thamani nchini kabla ya kusafirishwa nje ya nchi,” amebainisha Prof Kitila.


Soma zaidi: Miundombinu, madini vyachangia ukuaji wa uchumi wa asilimia 5.1 mwaka 2023 Tanzania


Kipaumbele hicho huenda kikaisaidia Serikali kunufaika na malighafi zinazozalishwa nchini ikiwemo madini ya kimakakati ikiwemo kinywe, Uraniamu na Tin ambayo tayari mchakato wa uvunaji wake umeanza.

Pia itaweka mazingira wezeshi yatakayovutia wawekezaji watakaojenga viwanda vya kuongeza thamani ya madini hapa nchini, hususan katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha betri za magari na mitambo.

Serikali pia itawekeza nguvu kaongeza upatikanaji wa raslimali watu wa kutosha na wenye ubora unaokidhi mahitaji ya dunia ya leo na kesho kupitia elimu na mafunzo mbalimbali yatakayoendelea kutolewa.

Tanzania itajiweka kwenye nafasi nzuri ya kuimarisha uzalishaji wenye tija kutokana na utajiri mkubwa wa rasilimali watu hususani vijana wenye umri chini ya miaka 35 ambao sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 inawataja kuwa asilimia 76 ya watu wote. 

Serikali kupitia mradi wa Jenga Kesho liyobora(BBT) imejipanga kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo yatakayoongeza uzalishaji wa malighafi kwa viwanda vya ndani na masokoya kimataifa.Picha/The Chanzo.

Kitila ambaye ni Mbunge wa Ubungo amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika ujenzi na utunzaji wa miundombinu.

Hili litafanyika kwa kushirikiana na sekta binafsi pamoja na kuimarisha uzalishaji wa nishati kama nyenzo muhimu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda, pamoja na kutekeleza kikamilifu mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Itakumbukwa kuwa Mei 8 mwaka hu Rais Samia Suluhu Hassan alizindua Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati ya Kupikia utakaowezesha kufikia asilimia 80 ya matumizi ya nishati hiyo kufikia mwaka 2030 ili kunusuru maisha ya watu yanayopotea kutokana ana athari za nishati chafu pamoja na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Pia Serikali pia itaendeleza na kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za kutosheleza za jamii na za kiuchumi zikiwemo afya, maji na umeme, barabara na mawasiliano hususan katika maeneo ya vijijini.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV