Maagizo ya Majaliwa kukuza uchumi wa Tanzania kwa lishe bora

November 18, 2021 2:44 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Amesema lishe bora ni muhimu kwawezesha watu kukuza uchumi.
  • Aagiza kasi ya kupambana na udumuvu iongezwe kwa watoto.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuendelea kulipa umuhimu wa kipekee suala la lishe nchini ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi imara kupitia maendeleo ya viwanda.

Majaliwa amesema lishe bora ndiyo msingi wa makuzi ya kimwili na kiakili kwa watoto na husaidia kuongeza uelewa kwa wanafunzi kuwa chanzo cha ubunifu katika kazi na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi.

“Maendeleo ya Taifa pamoja na mambo mengine, yanahitaji uwepo wa watu (nguvu kazi) wenye afya njema na lishe bora ili kuwawezesha kufanya kazi kwa bidii na tija. 

“Rasilimali watu imara ndiyo msingi wa kuzalisha kwa tija na kupunguza umaskini. Tutaendelea kuchukua hatua stahiki za kukabiliana na aina zote za utapiamlo,” amesema.

Waziri Mkuu aliyekuwa akizungumza Novemba 18, 2021 katika Mkutano wa Saba wa Wadau wa Lishe jijini Tanga amesema amesema lishe bora isipozingatiwa inasababisha udumavu wa kudumu kwa watoto na kuongeza mzigo wa gharama za matibabu kwa watoto na Taifa.

“Vilevile, lishe bora husaidia kuimarisha kinga na afya za watu na hivyo kuipunguzia Serikali mzigo wa gharama za matibabu kwa baadhi ya magonjwa pamoja na kuzisaidia kaya kupunguza mzigo wa gharama za matibabu au vifo miongoni mwa watoto, wanawake na watu wazima ambao ni nguvukazi,”

Kwa sasa, Tanzania inatekeleza mikakakati mbalimbali kuhusu lishe ikiwemo kuwa na mipango endelevu ya maendeleo ambayo inazingatia lishe kama moja ya vipaumbele ukiwemo Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano 

“Sekta binafsi ongezeni kasi katika uwekezaji wa uzalishaji wa vyakula vilivyorutubishwa pamoja na kuwekeza katika kuzalisha virutubishi nchini ili kupunguza gharama kubwa ya uagizaji wa virutubishi hivyo kutoka nje ya nchi.”

Aidha, Waziri Mkuu ameziagiza taasisi za elimu ya juu kuimarisha utafiti katika masuala ya lishe pamoja na kuhakikisha kuwa tafiti hizo zinatumika katika kutunga sera na kuelekeza afua za kimkakati za kupambana na utapiamlo.

Enable Notifications OK No thanks