Tanzania mbioni kuwa nchi inayoendelea

September 10, 2025 6:35 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Uamuzi huo umetokana na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Arusha. Tanzania imeorodheshwa kuwa miongoni mwa nchi zinazotazamiwa kutoka katika kundi la nchi maskini na kuwa nchi inayoendelea, hatua iliyochangiwa na maendeleo ya kasi katika sekta mbalimbali ikiwemo ya usafirishaji.

Uamuzi huo uliofanywa na Kamati ya Sera za Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UN) kupitia Shirika lake la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD) utaifanya Tanzania kukuza hadhi yake na ushawishi wa kisiasa katika majukwaa ya kimataifa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk Natu Mwamba aliyekuwa akizungumza wakati wa mkutano wa awali wa tathmini ya nchi kutoka nchi maskini kwenda nchi inayoendelea amesema uamuzi huo umetokana na maendeleo ya kiuchumi na kijamii yaliyopatikana nchini katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

“Pato la mtu kwa mwaka limeongezeka kutoka Dola za Marekani 453 mwaka 2000 hadi Dola 1,277 kwa mwaka 2023, kiwango cha umaskini uliokithiri kimepungua kutoka asilimia 36 mwaka 2000 hadi asilimia 26 mwaka 2024 kutokana na utekelezaji makini wa sera za fedha na ongezeko la mikopo kwa sekta binafsi”, alisema Dk Mwamba.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Awali wa Tathmini ya nchi kutoka nchi Maskini kwenda nchi inayoendelea inayofanywa na Umoja wa Mataifa (UN) kupitia Shirika lake la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD), wakifuatilia hotuba Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba.

Hii si mara ya kwanza kwa Tanzania kufikia mafaniko makubwa ya kiuchumi, mwaka 2020 Benki ya Dunia (WB) iliiiorodhesha Tanzania katika orodha ya nchi za uchumi wa kipato cha kati cha chini miaka mitano kabla ya kutimia kwa malengo iliyojiwekea.

Dk Mwamba amebainisha sababu nyingine kuwa ni udhibiti wa mfumuko wa bei uliosalia kuwa wa tarakimu moja, uwekezaji wa kimkakati ikiwemo mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere Hydropower (JHPP), mradi wa usafiri wa abiria na mizigo kati ya Dar es Salaam – Morogoro hadi Dodoma kupitia Reli ya Kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) na miradi ya sekta ya elimu na huduma za afya.

Aidha, Dk Mwamba ameishukuru timu ya wataalamu wa UNCTAD ambao tayari wameanza hatua za awali za tathmini ya nchi kutoka nchi maskini kwenda nchi inayoendelea na kuahidi Serikali kutoa ushirikiano thabiti ili kufanikisha zoezi hilo.

“Serikali ina imani na ziara hiyo ya wataalamu wa tathmini kwa kuwa pia itatoa mchango katika maendeleo ya nchi na kusaidia juhudi za Serikali za koboresha sera zitakazoifanya Tanzania kuwa imara zaidi, yenye usawa na mafanikio kwa wote,” amesema Dk Mwamba.

Kwa upande wake Shigeki Komatsubara, Mwakilishi Mkazi wa UNDP, amesema kuwa UN ipo tayari kuisaidia Tanzania kufanikisha kwa urahisi kuwa katika uchumi wa kati

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.