Tanzania kuomboleza kifo cha Malkia Elizabeth II kwa siku tano

September 10, 2022 7:55 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Bendera zote nchini na kwenye ofisi za balozi kupepea nusu mlingoti.
  • Rais Samia awaomba Watanzania kuungana na Waingereza kuomboleza.

Dar es salaam. Serikali ya Tanzania imetangaza maombolezo ya siku tano kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II wa Uingereza kilichotokea Septemba 8 mwaka huu huko Uskochi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyotolewa leo maombolezo yanaanza leo hadi Septemba 14, 2022.

Katika kipindi chote cha maombolezo bendera zote zitapepea nusu mlingoti nchini Tanzania pamoja na kwenye ofisi zake za balozi.

“Rais Samia amewaomba Watanzania wote kuungana na wenzetu wa Uingereza katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa kiongozi wao nchini humo,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia ya kifalme, Malkia Elizabeth amefariki kifo cha amani akiwa na umri wa miaka 96, baada ya kutawala kwa muda wa miaka 70 na kutajwa kuwa utawala mrefu zaidi katika historia.

Anatarajia kupumzishwa katika nyumba yake ya milele huko Westminister ndani ya siku 10 baada ya kifo chake. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Nukta TV

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Nukta TV

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Nukta TV