Mambo muhimu kuhusu Tanzania, Uingereza wakati wa utawala wa Malkia Elizabeth II

September 9, 2022 1:50 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Utawala wake uliwezesha Tanzania kupata uhuru kwa njia ya amani.
  • Alisaidia kupatikana kwa Katiba ya kwanza. 
  • Uingereza imekuwa mshirika muhimu wa maendeleo wa Tanzania.  

Dar es Salaam. Wakati dunia ikiomboleza kifo cha Malkia Elizabeth II kilichotokea Septemba 8, 2022  kwenye makazi yake Balmoral, Scotland, Tanzania itamkumbuka katika maeneo mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa Katiba kwanza na uhuru kwa njia ya makabidhiano ya amani.

Malkia Elizabeth alishikilia kiti cha enzi cha Uingereza Juni 2, 1953 kufuatia kifo cha baba yake Mfalme George VI  aliyetawala Tanganyika kama Eneo la Mamlaka ya Ligi ya Mataifa chini ya Uingereza kutoka Januari 10, 1920, alipokuwa na umri wa miaka 25 tu.

Baada ya kutawazwa kwake 1953, mwaka uliofuata, chama cha siasa cha Tanganyika African National Union (TANU) kiliundwa chini ya baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere kuongoza mapambano ya kudai uhuru.

Tanzania tofauti na nchi nyingine za Afrika ilipata uhuru mwaka 1961 kwa njia ya amani na majadiliano chini ya Serikali ya Malkia Elizabeth. Hii ilidhihirisha uongozi thabiti wa malkia na Mwalimu Nyerere.

Uingereza chini Malkia Elizabeth II, mwaka 1961 iliwezesha kupatikana kwa Katiba ya kwanza ya Tanganyika. 

Katiba hiyo, kwa kuzingatia mfumo wa Westminster, ilianzisha utawala wa kifalme wa kikatiba ambapo Malkia Elizabeth II ndiye akawa mkuu rasmi wa nchi, akiwakilishwa na Gavana Mkuu wakati mamlaka ya utendaji yalikabidhiwa kwa Waziri Mkuu Mwalimu Nyerere.

Hata hivyo, katiba hiyo haikuwa na muswada wa haki, ambao ulikuwa ni makubaliano ya Waingereza kwa Wazalendo wa Tanganyika. Harakati za kudai uhuru zilikuwa za ushirika, zikiendeshwa na vikundi vya kisiasa na vya kiraia vilivyounganishwa kwa karibu. 


Soma zaidi:

Disemba 9, 1961, Tanganyika ilipopata uhuru, moja kwa moja ikawa ni nchi ya  kifalme huku mfalme kikatiba akiwa ni Malkia wa Tanganyika, kabla ya Desemba 9, 1962 Tanganyika kuwa jamhuri yenye mfumo unaoongozwa na raisi.

Chini ya utawala wake, Uingereza ilitumia mfumo wa kuhamisha wafanyakazi wa mashambani, haki iliyosababisha kutokea kwa maeneo ya kikanda ya uagizaji na usafirishaji wa wafanyakazi na maeneo mengine kuachwa nje ya mchakato wa uhamiaji.

Mchango wake pia unakumbukwa kwa jitihada zilizofanywa kutoka miaka ya 1950 katika kuungana na maelfu ya wanafunzi, waelimishaji, watunga sera, wasomi, wabunifu na wajasiriamali kupitia Baraza la Uingereza Tanzania.

Malkia Elizabeth alitembelea Tanzania Julai 19 hadi 22, 1979, akitembelea Arusha, Dar es Salaam, Zanzibar, na Kilimanjaro kuimarisha mahusiano ya karibu na Uingereza.

Kwa sasa Uingereza ni mwekezaji mkubwa wa kigeni wa Tanzania na mfadhili wa pili kwa ukubwa baina ya nchi hizi mbili.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW