Rais Samia aungana na maelfu kumuaga Malkia Elizabeth II

September 19, 2022 12:20 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Anapumzishwa katika nyumba yake ya milele leo Septemba 19.
  • Rais Samia aungana na viongozi wa dunia kutoa heshima za mwisho.                

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ameungana na watu mashuhuri kutoka kote ulimwenguni kutoa heshima ya mwisho kwa Malkia Elizabeth II jijini London kabla ya kupumzishwa katika nyumba yake ya milele. 

Shughuli hiyo ya kumuaga Hayati Malkia Elizabeth II aliyetawala miaka 70 imefanyika huko Westminster Abbey.

Siku ya jumapili Rais Samia pamoja na viongozi wakuu wa kigeni takribani 500 walipata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa kusaini kitabu cha maombolezo kabla ya mazishi kufanyika kitaifa leo hii.

Tukio hili limekusanya maelfu ya watu waliomiminika katikati ya London usiku wa kuamkia leo huku baadhi wakishindwa kufika kutokana na kuharibika kwa miundombinu ya usafiri wa treni.

Katika shughuli hiyo Mfalme Charles III amewaongoza wanafamilia ya kifalme nyuma ya jeneza la Malkia Elizabeth II huku ulimwengu ukiendelea kumkumbuka kwa mchango wake wa kuimarisha amani na utulivu duniani.

Mfalme mpya ameambatana na ndugu zake Prince Anne, Prince Andrew na Prince Edward, wakati Prince William na Prince Harry wakiweka kando tofauti zao na kushiriki mazishi ya bibi yao. 


Soma pia

Wakati wa ibada ya mazishi, Askofu wa Canterbury amemsifu Malkia kwa “maisha tele na huduma ya upendo” na kuongeza “alikuwa na furaha, alipokuwa kwa wengi, akigusa maisha mengi.”

Malkia Elizabeth II anazikwa mahali pamoja na mpendwa wake Prince Philip, Duke wa Edinburgh, katika Kanisa la kumbukumbu la King George VI.

Inaaminika kuwa mazishi ya Malkia Elizabeth II yanakuwa “tukio kubwa zaidi la polisi kuwahi kufanywa” kwani mbali na maafisa 20,000 mjini London, wengine 2,300 wako kazini kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa Windsor mahali atakapozishwa. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV