Suluhu ya kuongeza ufaulu somo la hisabati Tanzania

January 17, 2022 1:51 pm · Maria
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya wanafunzi kidato cha nne kufeli vibaya.
  • Takriban wanafunzi 81 kati ya 100 wamefeli somo hilo.
  • Wadau washauri mitaala ifanyiwe marekebisho iweze kuendana na maisha ya wanafunzi na iwe ya vitendo zaidi.

Dar es Salaam. Wakati vicheko na maumivu vikiendelea kuhusu matokeo ya mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2021 yaliyotolewa hivi karibuni, mjadala wa kitaifa unahitajika kujadili namna ya kuongeza ufaulu katika somo la hisabati ambalo limewatoa jasho watahiniwa wa mtihani huo.

Kwa mujibu wa matokeo hayo yaliyotangazwa Januari 15 na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), asilimia 19.5 tu ya wanafunzi wote waliofanya mtihani huo ndiyo wamefaulu somo la hisabati (Basic Mathematics). 

Hiyo ni sawa na kusema kwa kila wanafunzi 100 waliofanya mtihani wa hisabati mwaka jana, takriban 81 wamefeli.

Ufaulu wa somo hilo kwa mujibu wa takwimu za Necta uko chini ya wastani wa kitaifa uliowekwa na baraza hilo kwa masomo ambao ni asilimia 50.

Ufaulu huo mbaya wa somo la hisabati siyo wa bahati mbaya kwa sababu kwa miaka mitano iliyopita ufaulu umekuwa chini ya wastani wa kitaifa kiasi cha wanafunzi kushindwa kuvuka hata robo ya ufaulu.

Wakati somo la hisabati likiwatesa zaidi wanafunzi, upande wa pili somo la Kiswahili limewatoa kimasomaso watahiniwa hao baada ya kufaulu kwa asilimia 95.5 au sawa na kusema kwa kila wanafunzi 10 basi tisa wamefaulu somo hilo.

Ufaulu wa Kiswahili ni karibu ya mara tano ya ule wa somo la hisabati, somo ambalo ni lugha ya Taifa na ambayo baadhi ya wachambuzi wa masuala ya elimu nchini, wamekuwa wakipendekeza itumike kama lugha ya kufundishia darasani ili kuwaongezea wanafunzi uelewa wa masomo.

Pia Kemia (Chemistry) ambalo ni miongoni mwa masomo ya sayansi, limekuwa somo la pili ambalo wanafunzi wamefaulu zaidi baada ya Kiswahili, ambapo ufaulu umefikia asilimia 92.1. 

Somo ambalo linatumika kama lugha ya kufundishia katika shule za sekondari la English Language (Kiingereza), wanafunzi wamefaulu kwa asilimia 66.8.

Civics ufaulu umekuwa asilimia 70.5, History (asilimia 59.2), Geography (asilimia 60.5), Biology (asilimia 67.2), Commerce (67.4) na Book Keeping kwa asilimia 71.3.


Soma zaidi:


Nini kifanyike?

Wakati wazazi na wanafunzi wakibaki na maswali juu ya ufaulu usioridhisha wa hisabati, wachambuzi wa masuala ya elimu wamependekeza ifanyike tathmini ya kitaifa ili kukusanya maoni yatakayobainisha kiini cha tatizo la wanafunzi kufeli somo hilo kila mwaka. 

Mwandishi wa vitabu mashuhuri, Richard Mabala amesema kutokana na kujirudia kwa hali ya kufeli somo la hisabati kwa miaka mingi, anaamini kuna haja kwa watunga sera kuangalia kuna tatizo gani katika mitaala na kama itawezekana itengenezwe upya kwa namna ambayo itaendana na maisha ya wanafunzi.

“Mitaala ni ya kinadharia sana kiasi kwamba wanafunzi hawaoni faida ya somo hilo kwao hali inayopelekea wao kutojighulisha kabisa na somo hilo,” amesema Mabala ambaye pia ni Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la HakiElimu ambalo linahusika na masuala ya elimu Tanzania. 

Mabala amesema ili mwanafunzi aweze kufaulu hesabu ni lazima ajue mantiki na mara nyingi wanafunzi wanashindwa kuona mantiki ya yale wanayoyakokotoa katika somo hilo.

Amesema wanafunzi wanapaswa kufundishwa matinki ambayo itaweza kuwasaidia siyo katika hesabu tu lakini pia hata katika masomo mengine.

Majibu hayo, kwa mujibu wa Mabala, yatasaidia katika utengenezaji wa mitaala rahisi itakayowasaidia wanafunzi kuongeza ufaulu wa somo hilo.

Suluhu nyingine itakayosaidia kuongeza ufaulu katika somo hilo, ni kubadili mtazamo miongoni mwa wanafunzi na walimu kuwa somo hilo ni gumu na lichukuliwe kama masomo mengine.  

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV