Ufaulu wa hisabati darasa la nne waimarika

Dar es Salaam.Ufaulu wa somo la hisabati kwa wanafunzi wa darasa la nne umeendelea kuimarika kwa miaka mitatu mfululizo suala linalotoa muelekeo chanya wa ubora wa elimu ya msingi nchini.
Kwa mujibu wa matokeo ya darasa la nne yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) Januari 10, 2026, asilimia 81.44 ya wanafunzi waliofanya mitihani wa hesabu mwaka 2025 wamefaulu.
“ “Somo la hisabati limeendelea kuimarika kwa ngazi ya darasa la nne kwani wanafunzi waliopata daraja E wamepungua kwa asilimia 10 na waliofaulu kwa daraja A wameongezeka kwa asilimia 10,” inaeleza taarifa ya Prof Mohamed.
Kwa takwimu hizo ni sawa na kusema wanafunzi 1,490,377 kati ya wanafunzi 1,583,686 walofanya mitihani hiyo Oktoba 22 na 23, mwaka 2025 wamefaulu.
Kutokana na ufaulu huo wanafunzi 8 kati ya kila 10 waliofanya mitihani hiyo wamefaulu somo la hisabati, suala linalotoa ahueni kwa walimu na wazazi ambao miaka ya nyuma walikuwa wakosota kutafuta suluhu ya kupandisha ufaulu wa somo hilo.
Kwa mujibu wa Necta, ufaulu huu wa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 10.04 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka 2024 ambao ulikuwa asilimia 71.4 huku mwaka 2023 ufaulu ukikuwa asilimia 54.
Hii inaashiria ongezeko la takribani asilimia 27 ndani ya kipindi cha miaka miwili, jambo linaloonyesha muelekeo chanya wa elimu ya msingi.
Latest