Simu za mkononi: Mbadala wa masanduku ya posta

May 5, 2022 1:00 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Zitatumika kuboresha masanduku hayo ya posta.
  • Vifurushi kuwafikia wateja popote walipo kwa kutumia simu za mkononi.

Mwanza. Huenda huduma za kupokea na kutuma barua na vifurushi zikamfikia kila mtumiaji wa simu Tanzania, baada ya huduma za posta kuunganishwa na mtandao wa simu nchini.

Shirika Posta Tanzania (TPC)  limesema kukamilika kwa usajili wa makazi kunaenda sambamba na uboreshaji wa anuani za masunduku ya posta ambapo namba za simu zitatumika kama mbadala wa anuani hizo.

Meneja wa TPC Mkoa wa Mwanza na Geita,  Dongwe James  akizungumza leo Mei 5, 2022 jijini Mwanza, amesema maboresho hayo yatarahisisha  shughuli za maendeleo  na kuimarisha ulinzi na usalama wa Taifa.

“Zamani watumiaji wa posta walikuwa wanaandika anuani ya posta pekee, hivi sasa tumeboresha kuendana na mabadiliko ya teknolojia,  mteja anapotuma bahasha yake posta ataandika anuani yake,  namba ya nyumba anayoishi na simu yake ya mkononi na mzigo wake atafikishiwa mpaka mlangoni,” amesema Dongwe.


Soma zaidi: 


Amesema anuani za makazi na ukuaji wa teknolojia ni muhimu kwa usalama wa Taifa na watumiaji wa huduma za posta kote duniani.

Meneja huyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa watendaji wanaotekeleza suala hilo ili kwenda sambamba na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha zoezi la anuani na makazi.

Wakizungumza na Nukta habari baadhi ya wakazi jijini Mwanza wamepongeza jitihada zinazofanywa na shirika hilo na kwamba zitasaidia katika kurahisisha utoaji wa huduma.

Abel  Nkurumba, mkazi wa jijini hapa amesema zaman walipopeleka mzigo au barua walilazimika kusubiri miezi au wiki ndipo mzigo ufike lakini hivi sasa ndani ya masaa 24 au 48 unapata mzigo wako.

“Huduma zimerahisishwa ni tofauti na zamani na hii ya anuani za makazi itaongeza urahisi wa mzigo au kifurushi kufika bila kupotea,” amesema Nkurumba.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV