Shilingi yaimarika dhidi ya Euro na Pauni, yabaki tulivu dhidi ya Dola

July 24, 2026 9:03 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Wafanyabiashara wanaotumia dola wataendelea kutumia kiwango sawa na kilichokuwa kinatumika tangu mwanzo wa wiki.

Dar es Salaam. Shilingi ya Tanzania imeendelea kuwa tulivu dhidi ya Dola ya Marekani huku ikiendelea kuimarika dhidi ya sarafu kadhaa ikiwemo Euro na Pauni ikilinganishwa na jana Alhamisi Julai 23.

Takwimu za viwango vya kubadilisha fedha vilivyotolewa katika benki za CRDB na NMB leo Julai 24, 2026 vinaonyesha kuwa Dola ya Marekani imeendelea kununuliwa Sh2,595 na kuuzwa kwa Sh2,675, hali inayoashiria utulivu wa sarafu hiyo katika soko la ndani. 

Hali hiyo pia inaendana na mwenendo wa soko la fedha ambapo Shilingi ya Tanzania imeendelea kubaki katika kiwango thabiti dhidi ya dola katika siku za hivi karibuni. 

Wakati benki ya CRDB ikitumia viwango sawa na jana kwa sarafu zote, NMB imepunguza kiwango cha kununua Euro kutoka Sh2,870 hadi Sh2,858 kwa euro moja, huku kiwango cha kuuza kikishuka kutoka Sh3,142 hadi Sh3,130. 

Hii ni punguzo la Sh12 kwa pande zote mbili, ishara kwamba euro imepungua thamani kidogo dhidi ya shilingi katika viwango vya benki hiyo.

Pauni ya Uingereza (GBP) nayo imeonyesha mwelekeo kama huo. NMB imenunua pauni kwa Sh3,322 badala ya Sh3,334 ya jana, huku bei ya kuuza ikishuka kutoka Sh3,679 hadi Sh3,666, sawa na punguzo la Sh12 hadi Sh13.

Kwa upande wa Sarafu za kikanda, NMB imepunguza kiwango cha kununua Shilingi ya Uganda kutoka Sh0.63 hadi Sh0.622 kwa kila shilingi ya Uganda, huku kiwango cha kuuza kikishuka kutoka Sh0.91 hadi Sh0.894 huku sarafu ya Kenya ikibaki tulivu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
24 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
24 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
24 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV

Kozi nzuri za kusoma chuo kikuu Tanzania

Kozi nzuri za kusoma chuo kikuu Tanzania

Nukta TV

Prof. Mbalawa, Waziri Misri wavutana, makubaliano ujenzi Bandari ya Bagamoyo

Prof. Mbalawa, Waziri Misri wavutana, makubaliano ujenzi Bandari ya Bagamoyo

Nukta TV