Shilingi tulivu dhidi ya Dola ya Marekani Mei 7, 2026
Viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni dhidi ya Shilingi ya Tanzania leo Mei 7, 2026 vimeonyesha mabadiliko madogo katika baadhi ya sarafu kuu za kimataifa ikilinganishwa na viwango vya jana, huku nyingine zikiendelea kubaki katika viwango vilevile.
Uchambuzi wa viwango vya kubadili fedha za kigeni vya benki kubwa za biashara nchini za CRDB na NMB, unabainisha kuwa Shilingi imeendelea kuwa tulivu dhidi Dola ya Marekani (USD).
Leo Dola ya Marekani imenunuliwa na CRDB kwa wastani wa Sh2,560 kutoka Sh2,570 ya jana, ikishuka thamani kwa Sh10. Aidha, Dola ya Marekani imeuzwa kwa Sh2,640 kutoka kutoka Sh2,650, hali inayoonyesha kuwa Shilingi inaendelea kuimarika kidogo kidogo.
Hata hivyo, katika Benki ya NMB, viwango vya Dola vimeendelea kubaki bila mabadiliko, ambapo inanunuliwa kwa Sh2,570 na kuuzwa kwa Sh2,650 kama ilivyokuwa jana.
Sarafu ya Umoja wa Ulaya (EUR) imeendelea kuimarika katika benki zote mbili. Katika Benki ya CRDB, inanunuliwa kwa Sh2,911.28 kutoka Sh2,896.21 ya jana, ikiwa ni ongezeko la Sh15.07 na kuuzwa kwa Sh3,211.28.
Kwa ujumla, mwenendo wa leo unaonyesha kuwa soko la fedha za kigeni nchini linaendelea kuwa tulivu, huku mabadiliko yanayoonekana yakibaki katika viwango vidogo.
Hali hii inaendelea kuwapa nafuu wafanyabiashara, wawekezaji na wasafiri wanaotegemea fedha za kigeni katika shughuli zao za kila siku, ikiwemo uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi, malipo ya ada za kimataifa pamoja na majukumu mengine ya kifedha.

Latest