Viwango vya kubadilisha fedha Tanzania Mei 8

May 8, 2026 12:09 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link

Viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni dhidi ya Shilingi ya Tanzania leo Mei 8, 2026 vimeonyesha mabadiliko madogo katika baadhi ya sarafu kuu za kimataifa ikilinganishwa na viwango vya jana, huku nyingine zikiendelea kubaki katika viwango vilevile.

Kupiitia benki ya CRDB na NMB Leo Dola ya Marekani imenunuliwa kwa wastani wa Sh2,560 na kuuzwa wa Sh2,640 ikiwa ni sawa na kiwango kilichorekodiwa jana hali inayoonesha utulivu katika soko biashara ya fedha za kigeni Tanzania.

Hata hivyo, uchambuzi uliofanywa na Nukta Habari unaonyesha mabadiliko kidogo ya shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani ndani ya mwezi mmoja.

Mwanzoni mwa Aprili Dola ya Marekani iliuzwa kwa Sh2,565 na kununuliwa kwa Sh2,645.

Mbali na Dola ya Marekani, sarafu nyingine ikiwemo ya Umoja wa Ulaya (EUR) imeendelea kuimarika katika benki zote mbili. Katika Benki ya CRDB, inanunuliwa kwa Sh2,915.37 kutoka Sh2,911.28 ya jana, ikiwa ni ongezeko la Sh4,09 na kuuzwa kwa Sh3,215.37.

Kwa ujumla, mwenendo wa leo unaonyesha kuwa soko la fedha za kigeni nchini linaendelea kuwa tulivu, huku mabadiliko yanayoonekana yakibaki katika viwango vidogo.

Hali hii inaendelea kuwapa nafuu wafanyabiashara, wawekezaji na wasafiri wanaotegemea fedha za kigeni katika shughuli zao za kila siku, ikiwemo uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi, malipo ya ada za kimataifa pamoja na majukumu mengine ya kifedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV