Dola ya Marekani, Shilingi ya Tanzania hali tulivu

April 20, 2026 5:11 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya viwango  vya ubadilishaji wa fedha hizo kutobadilika ndani a wiki moja.

Arusha. Soko la fedha za kigeni limeendelea kuwa tulivu nchini Tanzania baada ya viwango vya ubadilishaji wa Dola ya Marekani dhidi ya Shilingi ya Tanzania kubaki vilevile bila mabadiliko yoyote ikilinganishwa na wiki iliyopita.

Viwango vya kubadilisha fedha za kigeni dhidi ya Shilingi ya Tanzania vinavyotolewa na Benki za CRDB na NMB kwa matumizi ya leo Aprili 20, 2026 vinaonesha hakuna mabadiliko yoyote ikilinganishwa na wiki iliyopita.

Hali hiyo inaweza kuashiria utulivu wa soko la fedha za kigeni ambapo thamani ya Dola haijapata mabadiliko makubwa dhidi ya Shilingi ya Tanzania ndani ya kipindi hicho.

Kuanzia Februari 26 mwaka huu viwango vya kubadiili fedha za kigeni kupitia benki ya CRDB na NMB vilionesha kuimarika kwa Shilingi ya Tanzania suala lililotoa ahueni kidogo kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa nje ya nchi kwa kutumia Dola ya Marekani.

Leo Dola ya Marekani kupitia Benki ya CRDB imenunuliwa kwa Sh2,570 na kuuzwa kwa Sh2,650 ikiwa ni sawa viwango vilivyotumika wiki iliyopita.

Viwango hivi hubadilika kila siku kulingana na mwenendo wa soko la fedha, na vina umuhimu mkubwa kwa wafanyabiashara, wawekezaji na walipakodi, hasa katika kufanya malipo ya ada, kodi pamoja na ununuzi na uingizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

Kupitia viwango hivi vya kubadilisha fedha, watumiaji wa sarafu za kigeni hupata mwongozo sahihi wa kupanga bajeti, kufanya manunuzi na kuendesha shughuli zao za kifedha kwa ufanisi zaidi

Hata hivyo, Fedha nyingine kutoka mataifa mengine duniani zimeendelea kuimarika au kushuka kama inavyoonekana ikiashiria mabadiliko ya nguvu ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu za kimataifa.

/
No matches found for this filter
22 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
23 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
23 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA YA KIPOLISI ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI TANZANIA BARA 2025

MIKOA YA KIPOLISI ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI TANZANIA BARA 2025

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV

MIKOA 5 ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI 2025 TANZANIA BARA

MIKOA 5 ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI 2025 TANZANIA BARA

Nukta TV