Serikali yasisitiza kudhibiti bidhaa za nje, kulinda viwanda vya ndani

September 25, 2019 1:15 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizungumza na Balozi wa bidhaa za maziwa za ASAS na Msanii maarufu nchini, Mai Zumo wakati walipotemblea kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Picha|Ofisi ya Waziri Mkuu.


  • Imesema itaendelea kudhibiti  uingizwaji wa bidhaa mbalimbali kutoka nje ya Tanzania ili kulinda na kukuza viwanda vya ndani.
  • Hatua hiyo itasaidia kujenga uchumi wa viwanda na wa kati ifikapo 2025.

Dar es Salaam. Serikali imesema itaendelea kudhibiti  uingizwaji wa bidhaa mbalimbali kutoka nje ya Tanzania ili kulinda na kukuza viwanda vya ndani na vitakavyochangia ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyekuwa akizungumza leo (Septemba 25, 2019) katika ziara ya kikazi mkoani Iringa, amesema imani ya Serikali ipo kwenye uchumi wa viwanda. 

Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ineeleza kuwa endapo uchumi wa viwanda  ukiimarika uchumi wa nchi utakua kwa kasi na matokeo yake yataonekana hasa kwenye kuongeza wigo wa soko la ajira.

“Serikali imetoa wito kwa wawekezaji wawekeze katika viwanda mbalimbali nchini, hivyo ni muhimu wawekezaji hao wakalindwa na wasibugudhiwe ili waweze kuendelea na uzalishaji wa bidhaa zao,” amesema Majaliwa.


Zinazohusiana:


Aidha, Waziri huyo amesema sio ajira pekee itaimarika bali na mambo mengine yanayogusa nchi yakiwemo kupanua soko la huduma na shughuli za kiuchumi.

Sambamba na hayo, Majaliwa amewahakikishia wawekezaji wote kunufaika na uwekezaji wao huku akiipongeza kampuni ya Asas ya mkoani Iringa kwa kutoa elimu kwa wafugaji juu ya namna bora ya ufugaji ikiwa ni pamoja na kufuata kanuni bora za ufugaji wa kisasa pamoja na kuwapa uhakika wa soko.

Tangu alipoingia madarakani mwaka 2015, Rais John Magufuli amekuwa akihubiri uchumi wa viwanda ili kiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025.

Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha maziwa cha Asas, Fuad Abri amesema kiwanda chao kina mpango wa kupanua uzalishaji ambapo kinaendelea na ujenzi wa kiwanda kingine cha usindikaji maziwa kilicho kwenye hatua za mwisho za kukamilika wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Nukta TV

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV