Serikali yajibu uhaba wa wataalamu wa ganzi, usingizi

September 1, 2026 2:07 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya siku ya mwaka mmoja, miezi minane na siku 20 tangu Nukta Habari kuonyesha tatizo hilo kupitia makala yake.

Dar es Salaam. Baada mwaka mmoja na miezi nane tangu Nukta Habari iangazie uhaba wa wataalamu wa usingizi na ganzi unaohatarisha huduma za upasuaji nchini, Serikali imesema imetenga ajira mpya za kada hizo za afya ili kukabiliana na uhaba wa wataalamu hao nchini.

Desemba 12, 2024, Nukta Habari ilichapisha makala maalum iliyoelezea uhaba wa watalaamu wa ganzi na usingizi waliopo katika mfumo rasmi wa ajira na wale waliopo vyuoni changamoto wanazopitia licha ya kuwa muhimu katika kuokoa maisha ya watu katika vyumba vya upasuaji.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Ndege aliyekuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mbulu Vijijini, Dk Emmanuel Nuwas leo, Septemba 1, 2026, bungeni jijini Dodoma, amesema Serikali imetenga ajira mpya 10,009 kwa kada mbalimbali za afya.

“Serikali imetenga katika bajeti yake kuajiri watumishi katika ajira mpya 10,009 kwa maana kwamba katika kada zote za afya lakini kuhakikisha kwamba tunapata watu wataalam wa ‘technologist’ ambao watakuwa takriban zaidi ya 200,” ameeleza Naibu Waziri Ndege.

Majibu hayo yamekuja baada ya Dk Nuwasi kuhoji bungeni ni upi mpango wa Serikali kuajiri wataalam wa mionzi lakini pia wa dawa za usingizi na ganzi ili kupeleka huduma za upasuaji karibu na wananchi katika halmashauri na vituo vya afya nchini.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, sehemu ya ajira hizo inalenga kupata wataalamu wa teknolojia za afya ambao watapangiwa katika vituo vya afya na hospitali za wilaya.

Ndege amebainisha kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa Serikali kuhakikisha uwekezaji uliofanyika katika miundombinu na vifaa tiba unaenda sambamba na uwepo wa watumishi wenye uwezo wa kutoa huduma.

Tatizo hilo limekuwa likiibua maswali kuhusu uwezo wa mfumo wa afya kukidhi mahitaji ya wananchi, hasa katika maeneo ambayo huduma za kibingwa bado hazipatikani kwa urahisi.

Kwa mujibu wa makadirio ya idadi ya watu ya mwaka 2026 ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Tanzania ina zaidi ya watu milioni 70.

Idadi hiyo inaendelea kuongezeka, jambo linaloongeza mahitaji ya huduma za afya, ikiwamo upasuaji na huduma za ganzi.

Shirikisho la Vyama vya Madaktari wa Usingizi na Ganzi Duniani (WFSA) linapendekeza daktari mmoja wa usingizi na ganzi kuhudumia watu kati ya 20,000 na 25,000.

Hali hiyo inaifanya ajira na usambazaji wa wataalamu wa kada hiyo kuwa suala muhimu katika kuhakikisha upasuaji unafanyika kwa usalama katika hospitali na vituo vya afya.

Serikali yasema stahiki zinaendelea

Mbali na suala la ajira, Naibu Waziri amefafanua kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuboresha mazingira ya watumishi wa kada za afya kwa kuhakikisha wanapata stahiki na motisha mbalimbali. 

Miongoni mwa motisha hizo ni pamoja na posho za kufanya kazi za ziada (on-call allowance), posho za sare na posho za uchunguzi wa maiti ambazo wataalamu wa afya wamekuwa wakizipigia chapuo mbalimbali.

Uchache wa madaktari hao unachochea wagonjwa wanaopaswa kupewa dawa za usingizi na maumivu hususan wale wanaofanyiwa upasuaji nchini kuwa hatarini kupoteza maisha. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
1 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
1 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Leseni mpya bandari kavu zasitishwa Dar es Salaam

Leseni mpya bandari kavu zasitishwa Dar es Salaam

Nukta TV

Matarajio ya wachambuzi wa siasa na uchumi kwa Ndejembi

Matarajio ya wachambuzi wa siasa na uchumi kwa Ndejembi

Nukta TV

Maagizo mazito ya Rais Samia kwa Ndejembi

Maagizo mazito ya Rais Samia kwa Ndejembi

Nukta TV