Serikali yaanza kutafuta suluhu Watanzania kutoingia Marekani

June 18, 2025 6:18 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Yasema itoa taarifa zaidi kadri mazungumzo yanavyoendelea.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema imeanza mazungumzo na Marekani ili kushughulikia changamoto zinazoweza kuzuia Watanzania kuingia nchini humo.

Uamuzi huo unatokana na Serikali ya Marekani kutoa orodha ya nchi 36 baadhi yake kutoka barani Afrika ikiwemo Tanzania ambazo raia wake wanaweza kukutana na marufuku kuingia nchini humo.

Taarifa ya zuio hilo la Serikali ya Marekani inayoongozwa na Rais Donald Trump ilitolewa hivi karibuni ikihusisha nchi 25 za Afrika, ilidai kutaka kuchukua hatua hiyo kwa kile ilichokieleza udanganyifu wa taarifa za raia wa nchi hizo.

Taarifa iliyotolewa leo Juni 18, 2025 na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, kupitia ukurasa wake wa Instagram, imeeleza kuwaTanzania imeona tangazo la Serikali ya Marekani la kutaka kufanyiwa kazi kwa mambo kadhaa ya kiuhamiaji ambayo yanaweza kusababisha raia wa Tanzania kuzuiwa kuingia Marekani.

“Naomba kuujulisha umma kuwa tayari Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imeanza kufanya mashauriano na wenzetu upande wa Marekani kujua maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa maboresho hususani yanayohusiana na masuala ya kikonseli,” amesema Msigwa.

Miongoni mwa sababu zilizotajwa na Serikali ya Marekani za kutakiwa kufanyiwa kazi na mataifa 36 ni pamoja na kukosa ofisi rasmi inayotoa nyaraka za utambulisho kwa raia wake na kushamiri kwa udanganyifu kwenye mchakato wa utolewaji nyaraka za utambulisho. 

Rais wa Marekani Donald Trump tangu aingie madarakani amekuwa akifanya maboresho ya Sera mbalimbali za nchi hiyo ikiwemo kufuta misaada iliyokuwa inatolewa na Shirika la Misaada la Marekani la USAID katika nchi mbalimbali duniani.

Mambo mengine ambayo Trump amezuia ni pamoja na ufadhili wa dawa za Ukimwi, kulazimisha kujisajili wahamiaji bila stakabadhi, kupunguza haki za umma kwa wahamiaji, pamoja na kusitisha amesitisha upatikanaji wa uraia kwa watoto waliozaliwa Marekani kwa wazazi wasio raia na ambao hawawezi kuthibitisha uraia wa baba.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV