Serikali ya Tanzania yafunga vituo 74 vya kutibu corona

July 3, 2020 3:18 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema pamoja na kwamba ugonjwa huo upo ukingoni bado jamii na watumishi wa afya hawapaswi kubweteka.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imefunga vituo 74 vya kuhudumia wagonjwa wa virusi vya corona kati ya 85 vilivyokuwa vimeandaliwa baada ya kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo kupungua.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amefunga kituo cha 74 Ijumaa (Julai 3, 2020) kilichokuwepo katika Hospitali ya Lulanzi na kukikabidhi kwa Halmashauri ya Mji wa Kibaha  huku akiwataka wakazi wa mji huo kutohofia kwenda kupatiwa matibabu kama hospitali nyingine.

Wizara hiyo hiyo imesema kituo hicho cha Lulanzi kilikuwa ni moja ya vituo vikubwa nchini vilivyokuwa vimeandaliwa kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa virusi vya corona kikiwa nyuma ya Amana, Mloganzila na Temeke.

Mgonjwa wa mwisho katika kituo hicho kwa mujibu wa Ummy aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo Mei 26 mwaka huu.


Zinazohusiana


“Tunashukuru mwenyezi mungu kuwa Ugonjwa wa corona unaelekea mwishoni mwishoni kutoweka Tanzania. Tulikuwa na kambi 85 lakini leo zimebaki 11 tu ikiwemo hospitali binafsi,” amesema Ummy.

Waziri huo amesema kuwa pamoja na kwamba ugonjwa huo upo ukingoni bado jamii na watumishi wa afya hawapaswi kubweteka kwa kuwa kuna wasiwasi wa kutokea wimbi la pili la ugonjwa huo.

“Tuendelee kuhamasisha kuhimiza masuala ya kujikinga dhidi ya virusi hivyo,” amesema Ummy.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tanzania ina visa vya wagonjwa wa corona 509 na vifo 21.

Katikati ya Juni, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alibainisha kuwa hadi Juni 15 Tanzania ilikuwa na wagonjwa 66 pekee wa corona katika mikoa 10 huku 16 ikiwa haina mgonjwa kabisa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

Nukta TV

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

Nukta TV

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Nukta TV