Serikali kuitua mzigo wa madeni, tozo ATCL Tanzania

April 22, 2021 2:13 pm · Nuzulack Dausen
Share
Tweet
Copy Link
  • Litaendeshwa kimkakati ii liweze kujiendesha kwa ufanisi na kulipunguzia hasara.
  • Serikali italitua mzigo wa madeni makubwa na kulipa ahueni ya baadhi ya tozo na kodi.
  • Rais Samia amesema ATCL itafanyiwa marekebisho makubwa ili ijiendeshe kibiashara. 

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali yake itaendelea kulilea Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kimkakati ii liweze kujiendesha kwa ufanisi ikiwemo kulitua mzigo wa madeni makubwa na kulipa ahueni ya baadhi ya tozo na kodi. 

Rais Samia ameliambia Bunge leo Aprili 22, 2021 jijini Dodoma kuwa hatakubali kuona ATCL inapata hasara licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali. 

“Naposema kimkakati ni pamoja na kuangalia kutoa unafuu wa madeni na baadhi ya kodi na tozo kama inavyofanyika kwenye nchi nyingine ili liweze kukua na liweze kuweka mahesabu sawa,” amesema kiongozi huyo.

Hatua hiyo itaisadia ATCL kuweza kupunguza gharama ya matumizi na sahara inayoikabili.


 Soma zaidi: 


Hivi karibuni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere alisema ATCL ilipata hasara ya Sh60 bilioni katika mwaka wa fedha 2019/20 na kwamba miaka yote mitano pia ilipata hasara. 

Rais amesema kwa sasa shirika  linasomeka kuwa na hasara kwa sababu ya kurithi madeni ya nyuma. 

“Tutajitahidi kusoma mwenendo wa biashara ya ndege ulimwenguni…hatutakubali kuona Shirika linaendelea kupata hasara baada ya uwekezaji mkubwa tuliofanya,” amesema na kuongeza kuwa wataenda kulifanyia uchambuzi wa kina na kuhakikisha kuwa watakaoachiwa kuliendesha ni wale wenye weledi na uwezo wa kuliendeleza. 

Hata hivyo, Rais Samia hakuweka bayana kiwango cha madeni ambacho Serikali watayapunguza na aina za tozo ambazo ATCL inadaiwa. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV