Sababu mwandishi wa TBC kufariki akishuka Mlima Kilimanjaro

December 14, 2022 12:33 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Kifo hicho kimetokana na ajali ya baiskeli aliyokuwa akiendesha wakati akishuka mlima huo.
  • Alifariki wakati ametoka katika uzinduzi wa intaneti kwenye kilele cha mlima huo.

Dar es Salaam. Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limesema kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Joachim Kapembe kimesababishwa na ajali ya baiskeli iliyotokea ndani ya hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.

Kifo cha  Kipembe (45) kimetokea Disemba13, 2022 majira ya saa 12:00 jioni katika kituo cha Kibo (Kibo Hut) kuelekea kituo cha Horombo.

“Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya  Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) iliyopo Moshi.,” imesema taarifa ya Tanapa iliyotolewa na leo Disemba 14, 2022 na kusainiwa na Afisa Mwandamizi wake Catherine Mbena. 

Kapembe ambaye enzi za uhai wake alikuwa mtumishi wa TBC alikuwa mmoja kati ya watu waliopanda Mlima Kilimanjaro Disemba 13, 2022 wakati wa kwenda kuzindua mtandao wa intaneti katika kilele cha Uhuru.


Soma zaidi


Huduma hiyo ya intaneti ilizinduliwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ambapo inatajwa itarahisisha upatikanaji wa mawasiliano ya kimtandao kwenye mlima huo, mrefu kuliko yote Afrika.

Hatua hiyo inaelezwa kuwa inaweza kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea mlima huo kwa shughuli za utalii na hivyo kuongeza mapato kwa Serikali na ajira kwa watu wakiwemo waongoza watalii. 

“Tunataka tuangaze sana, tuconnect (tuunganishe) kilele kikubwa sana cha bara letu na wote watakaokuja kutembelea…nataka tukio hili litumike kuwafanya Watanzania wajivunie nchi yao,” alisema Nape kwenye hafla iliyoandaliwa kabla ya kupanda mlima huo. 

Waziri Nape aliongozana na viongozi mbalimbali kwenye uzinduzi huo akiwemo Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, wanahabari, timu ya madtari, wapagazi na watalii wengine kutoka ndani na nje ya nchi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV