Ripoti: 46% ya  wanawake Tanzania wakabiliwa na vikwazo vya kiuchumi 

October 8, 2026 8:10 am · Method Allen
Share
Tweet
Copy Link
  • Sababu zikiwa ni kujikita zaidi katika shughuli zenye tija ndogo na upatikanaji mdogo wa mitaji.

Dar es Salaam. Serikali na wadau wa maendeleo huenda wakatakiwa kuongeza nguvu katika kuwawezesha wanawake kiuchumi, baada ya ripoti mpya kubaini bado wanakabiliwa na vikwazo vinavyopunguza tija ya shughuli zao.

Ripoti mpya ya hali ya uchumi Tanzania ya Septemba 2026 inayottolewa na Benki ya Dunia (WB)  inabainisha kuwa karibu nusu ya kundi hilo bado llinakabiliwa na vikwazo vya kiuchumi.

“Mwenendo kama huo unaonekana pia katika biashara ndogo zinazoongozwa na wanawake, ambazo zina uzalishaji kwa wastani ulio chini kwa asilimia 46 ikilinganishwa na biashara zinazoendeshwa na wanaume,” inaeleza ripoti ya Benki ya Dunia.

Kwa upande wa biashara ndogo ndogo ‘micro business’ ambazo nyingi zinaendeshwa na wanawake zina faida kwa kiwango cha chini ikikadiriwa kuwa ni takribani asilimia 46 ikilinganishwa na zile za wanaume. | Picha Canva

Ripoti inaeleza kuwa pengo hilo linahusishwa na sababu mbalimbali, ikiwemo wanawake kujikita zaidi katika shughuli zenye tija ndogo, upatikanaji mdogo wa mitaji na mapato madogo yatokanayo na mali.

Pamoja sababu hizo Benki ya Dunia pia imeutaja mzigo wa malezi kuwa mingon mwa sababu nyingine zinazozuia ukuaji wkaiuchumi wa wanawake.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanawake hutumia takribani asilimia 14 ya muda wao katika kazi za nyumbani na malezi yasiyolipwa, zaidi ya mara tatu ya asilimia nne inayotumiwa na wanaume.

Hali hiyo inachangia kile Benki ya Dunia inachokiita umaskini wa muda ‘timely poverty’ ambapo majukumu mengi ya kifamilia huwaacha wanawake na muda mchache wa kushiriki katika shughuli zinazoweza kuongeza kipato na tija.

Wachambuzi waeleza suluhu

Nukta Habari imezungumza na wachambuzi wa masuala ya uchumi ili kujua hatua zinazopaswa kuchukuliwa kuwaondoa wanawake katika vikwazo vya kiuchumi vinavyowakabili.

Wanawake wana uwezekano wa mara mbili zaidi kufanya kazi kama wasaidizi wa familia bila malipo, kundi linalounda asilimia 35 ya wafanyakazi wote wa sekta ya kilimo | Picha Canva

Mchambuzi wa masuala ya uchumi, Paul Chegula, anasema ili kuwaondoa wanawake katika vikwazo hivyo, ni muhimu kukabiliana na tamaduni zisizofaa, ikiwemo mfumo dume, huku Serikali ikiweka mazingira yenye fursa sawa katika maeneo mbalimbali.

“Kuweka fursa sawa upande wa Serikali katika maeneo mbalimbali, maeneo ya ajira, maeneo ya elimu na kadhalika. Kwamba hata kwenye upande wa ajira usiwe na vigezo, tuweke fursa sawa ili nao wakiweza kuingia kwenye soko la ajira wanaweza waka-boost uchumi wao,” amesema Paul.

Chegula ameongeza kuwa uwezeshaji wa wanawake hauwezi kutenganishwa na elimu, akisisitiza umuhimu wa familia kuwapa watoto wa kike fursa sawa za elimu kama watoto wa kiume.

“Kwenye eneo la elimu, wazazi, familia, mambo ya kusomesha mtoto wa kiume pekee zimeshapita. Tukiwawekea nguvu hawa wamama wana uwezo mkubwa sana wa kuweza kubadilisha jamii na hali za kiuchumi zao zitabadilika kabisa,” amesema.

Kwa upande wake, Dk Lenny Kasoga, mtaalamu wa uchumi kutoka Mwanza, akizungumzia namna majukumu ya malezi yanavyoweza kuwabana wanawake kiuchumi na kijamii, amesisitiza umuhimu wa kuanzisha mijadala ya kijamii kuhusu changamoto hizo.

“Kama jamii tuanze kuweka midahalo ambayo watu watapata kujadili, kwa sababu watu wengine sasa hivi hawana muda wa kujadili. Wanawake wanahangaika sana, maanake mwanamke hawezi kukataa kuwa mwanamke, maana anazaa, akishazaa lazima alee. Kitu ambacho kinabidi kiwekewe mkazo ili kijadiliwe na watu,” amesema.

Kasoga anasema mijadala hiyo inaweza kusaidia jamii kutafakari namna ya kupunguza mzigo wa majukumu ya malezi kwa wanawake na kuweka mazingira yatakayowawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Dk. Ndumbaro: Suala la utawala bora watu wanaliangalia kwa mtazamo finyu.

Dk. Ndumbaro: Suala la utawala bora watu wanaliangalia kwa mtazamo finyu.

Nukta TV

Kama huingizi angalau Sh750,000 kwa mwezi, hii inakuhusu

Kama huingizi angalau Sh750,000 kwa mwezi, hii inakuhusu

Nukta TV

Ujumbe mzito wa Dk. Tulia Ackson kuhusu usawa akiaga urais wa IPU

Ujumbe mzito wa Dk. Tulia Ackson kuhusu usawa akiaga urais wa IPU

Nukta TV