Saba wateuliwa kinyang’anyiro cha kumrithi Dk Tedros WHO 

October 30, 2026 3:45 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Bodi ya Utendaji ya WHO itachuja wagombea saba na kupendekeza hadi majina matatu kwa ajili ya uteuzi wa mwisho.
  •  Atakayechaguliwa ataanza rasmi majukumu Agosti 16, 2027.

Dar es Salaam. Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza wagombea saba waliopendekezwa na nchi wanachama kuwania nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo atakayechukua nafasi ya Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus, anayemaliza muda wake Agosti 2027.

Taarifa ya WHO iliyotolewa Oktoba 29, 2026, inabaiNisha kuwa wagombea hao walioteuliwa ni pamoja na Dk Hanan Mohammed Al-Kuwari kutoka Qatar.

Wengine walioteuliwa ni Dk Hanan Balkhy kutoka Saudi Arabia, Dk Hans Henri P. Kluge (Ubelgiji , Dk María P. Neira (Hispania ), Dk Budi Gunadi Sadikin [Indonesia] , Dk Li Song (China) na Dk Gevorg Tamamyan ( Botswana).

Wagombea hao wanatarajiwa kukutana na nchi wanachama na washirika wa WHO Novemba 18 na 19, 2026, katika jukwaa la kwanza la wagombea litakalofanyika makao makuu ya shirika hilo jijini Geneva, Uswisi.

Hatua itakayofuata ni kukutana kwa Bodi ya Utendaji ya WHO mapema mwaka 2027 ili kuchagua majina matatu yatakayowasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Afya Duniani.

Mkutano huo, ambao ni chombo kikuu cha maamuzi cha WHO, unatarajiwa kumteua Mkurugenzi Mkuu mpya katika kikao chake cha 80 mwezi Mei 2027. Atakayeibuka mshindi anatarajiwa kuanza rasmi majukumu yake Agosti 16, 2027.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO ajaye atahudumu kwa vipindi viwili vya miaka mitao mitano iyajo kabla ya kuachia kijiti kwa kiongozi mwingine atakayechaguliwa.

Historia ya Dk Tedros itajirudia?

Dk Tedros aliyekalia kiti cha WHO kwa vipindi viwili tangu mwaka 2017 anaondoka madarakani akiacha historia ya kuwa Mwafrika wa kwanza kutoka Kanda ya Afrika ya WHO kuongoza shirika hilo.

Kiongozi huyo mwenye asili ya Ethiopia alipokea kijiti kutoka kwa mtangulizi wake Dk Margaret Chan kutoka China, aliyengoza kuanzia Januari 1, 2007.

Katika uongozi wake WHO, Dk Tedros aliongoza uratibu wa WHO katika kukabiliana na janga la UVIKO-19, ikiwemo kutangaza mlipuko huo kuwa Dharura ya Afya ya Umma yenye umuhimu wa Kimataifa Januari 2020. 

Aidha, alisimamia mpango wa kimataifa wa Triple Billion Targets uliolenga kupanua upatikanaji wa huduma za afya kwa wote, kuimarisha maandalizi ya kukabiliana na dharura za kiafya na kuboresha ustawi wa watu. 

Katika uongozi wake, WHO pia iliendelea kuratibu mapambano dhidi ya magonjwa ya kuambukiza yakiwemo Ebola, huku ikiimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na milipuko ya magonjwa na kutafuta ufadhili endelevu wa shughuli zake. 

Upande wa kushoto ni Dk Gevorg Tamamyan wa Botswana, mmoja wa wagombea saba waliopendekezwa kuwania nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Picha| WHO.

Kwa sasa jicho la Waafrika lipo kwa Dk Gevorg Tamamyan ambaye ndiye mgombea pekee kutoka bara la Afrika anayetokea nchini Botswana.

Iwapo Dk Gevorg Tamamyan akishinda atakuwa boss wa nane wa WHO tangu kuanzishwa kwake April 7,1948.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
30 Oct, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Tanzania na Angola kuunganisha reli na safari za ndege

Tanzania na Angola kuunganisha reli na safari za ndege

Nukta TV

Tanzania kufungua tena ubalozi Angola, Balozi mpya kuteuliwa

Tanzania kufungua tena ubalozi Angola, Balozi mpya kuteuliwa

Nukta TV

Makonda: 28 - 30 Oktoba ni siku za kumshukuru Mungu kwa kuitunza amani ya Tanzania

Makonda: 28 - 30 Oktoba ni siku za kumshukuru Mungu kwa kuitunza amani ya Tanzania

Nukta TV