‘RevEye Search’: Programu inayoweza kukusaidia kupambana na uzushi wa Corona

November 30, 2020 8:03 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Inapatikana kwenye kitafutio cha Google Chrome  ili uweze  kuitumia na  kupata kiunganishi ( RevEye Image Search).
  • Inatumika kuhakiki habari iliyotolewa kwa mfumo wa picha.
  • Ni programu muhimu katika mapambano dhidi ya Corona.

Dar es Salaam. Vita dhidi ya habari za uzushi hasa zinazohusu ugonjwa wa Corona inaendelea kushika kasi. Kila mahali ni mashambulizi, kuhakikisha dunia inatoka salama kwenye janga hilo.

Teknolojia nayo inatumika kikamilifu kuwaelimisha na kuwawezesha watu kutumia programu za kidijitali kung’amua na kisha kutokomeza kila uzushi uongo unaoibuka kuhusu COVID-19.

Moja ya programu hizo za kidijitali ni  RevEye Image Search ambayo husaidia kuthibitisha habari iliyopo kwenye mfumo wa picha.

Ili uweze kutumia programu hiyo kwa mwanahabari au mtu yoyote unatakiwa uwe na kompyuta  ambayo ina kitafutio cha Google Chrome ambacho kinaendeshwa na kampuni ya Google.

Nenda kwenye kitafutio hicho na tafuta neno “RevEye Image Search plugin” na fuata maelekezo yote. Ukishaipata na kuifungua utakutana itakuekeleza kuiweka rasmi kwenye Google Chrome, tayari kwa matumizi yako.


Zinahusiana:


Jinsi RevEye Image Search inavyofanya kazi

Ili kutumia programu hiyo, unatakiwa kwenda kwenye habari picha kisha bonyeza upande wa kulia (right click) wa kipanya (mouse) cha kompyuta yako baada ya hapo atakutana na machaguo zaidi ya manne ya jinsi ya kuthbitisha habari picha hiyo.

Machaguo hayo ni Google search, RevEye Search , Bing Image Match, Yandex Search na Baid Search ambapo hutumika katika uthibitishaji habari.

Chagua RevEye Search ili kupata majibu ya picha husika na utaweza kufahamu kama habari hiyo ina potosha.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
30 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Vodacom Tanzania yapendekeza gawio la Sh23.91 kwa hisa 2026

Vodacom Tanzania yapendekeza gawio la Sh23.91 kwa hisa 2026

Nukta TV

Fursa kwa wakulima, uhitaji mazao ya chakula ukiongezeka Kenya, Uganda

Fursa kwa wakulima, uhitaji mazao ya chakula ukiongezeka Kenya, Uganda

Nukta TV

Jinsi afya ya akili inavyowatesa wanawake makazini

Jinsi afya ya akili inavyowatesa wanawake makazini

Nukta TV