Undani wa habari zinazopotosha kuhusu COVI-19

January 2, 2021 11:46 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Zinakuja kwa mtindo mbalimbali ikiwemo upotoshaji wa maudhui (Misleading content).
  • Misleading Content ni pale mtu anapochukua sehemu ya nukuu ambayo anaikusidia yeye na kuacha sehemu nyingine ya nukuu kwa nia ya kupotosha.
  • Kabla ya kusambaza habari picha au takwimu ujiulize habari hiyo ina ukweli kiasi gani.

Dar es Salaam. Ukuaji wa teknolojia umefanya habari nyingi kupatikana kwa urahisi na kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja lakini kwa upande mwingine umesababisha kuongezaka kwa wimbi la taarifa za uzushi na uongo hasa wakati wa majanga kama ugonjwa wa COVID-19.

Miongoni mwa habari hizo za uzushi ni zile zinakuja na maudhui yanayopotosha (misleading content) ambazo mara nyingi zimekuwa zikileta taharuki na madhara kwenye jamii.

Aina hii ya habari ya upotoshaji imekuwa  zikitumika kwa nia ovu na mara nyingine  bila kujua kuwa habari husika ni ya kupotosha.

Mfano wa “misleading content” ni pale mtu anapochukua sehemu ya nukuu iliyopo kwenye habari ambayo anaikusidia yeye na  kuacha sehemu nyingine ya nukuu kwa nia ya kupotosha au kutumia sehemu ya takwimu kwa ajili ya manufaa yake bila kuleza hizo takwimu zimepatikanaje.

Wakati mwingine kuchukua hata picha na kuchukua kipande cha picha na kukionyesha katika habari yake sambamba na kukiongezea maneno mengine  kwa nia ovu ya kumuumiza muhusika mwingine.


Zinazohusiana:


Aina hii ya upotoshaji imekua ikitumika zaidi kuzua taharuki hasa za virusi VYA covid-19 ili kuwaumiza watu kwenye jamii. Kwa mfano mwisho mwa mwaka 2020, watu wenye nia ovu walitumia picha ya Meya wa London wa Uingereza, Sadiq Khan aliyopigwa wakati anapata chanjo ya mafua na kuitumia kuwa alikua anapata chanjo dhidi ya Corona.

Ili kuibaini aina hiyo ya habari ya upotoshaji unahitaji kutumia zana za kidijitali ikiwemo ‘Google Image Explore’ ambazo zinasaidia kukufahamisha uhalali wa habari au picha na ilikochukuliwa.

Pia ukipata habari ambayo unafikiri una mashaka nayo, usiisambaze kwa haraka, jipe muda wa kutafuta ukweli wake ili kupunguza madhara ya habari za uzushi kwenye jamii hasa wakati huu dunia ikipambana na janga la Corona.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.