Yandex: Zana ya kidijitali kukabiliana na uzushi wa Corona

February 4, 2021 8:33 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni programu inayosaidia kung’amu ukweli kuhusu habari picha zenye mashaka.
  • Inaweza kubaini picha mtandaoni au zilizopo kwenye kifaa chako cha siku au kompyuta.
  • Programu hiyo inawafaa wathibitishaji wa habari wa kiwemo wanahabari.

Dar es salaam. Kama bado unapata shida ya kutofautisha habari picha ya kweli ya uongo hasa zinazohusu janga la COVID-19, basi usiwe na shaka maana teknolojia inakupatia suluhisho bila kulipigia gharama yoyote. 

Moja ya teknolojia hizo ni matumizi ya programu ya ‘Yandex’ ambayo inaweza kufahamu kwa undani matumizi na historia za picha zinazotumika mtandaoni. 

“Yandex” ni kitafutio cha taarifa kama ilivyo kwa Google ya Marekani lakini tofauti yake hii inatokea nchini Urusi. Unawezaje kutumia kitafutio hicho ukapata matokeo mazuri ya picha yoyote hata zinazohusu COVID-19? Fuata hatua hizi kujifunza zaidi:

Nama ya kutumia ‘Yandex’

Hatua ya kwanza, mara baada ya kupata picha mtandaoni au uliyoitilia shaka unatakiwa  kwenda kwenye mtandao wa Google kisha tafuta neno ‘images.yandex.com’

Hatua ya pili utabonyeza kamera iliyopo upande wako wa kulia wa sehemu ya kitafutio cha  Yandex.

Hatua ya tatu ni kupakia picha hiyo (uploading) au kupitia kiungaishi (link) kwenye mtandao huo ili kufahamu ukweli kuhusu picha unayoitilia mashaka.


Zinazohusiana:


Picha hiyo ikiingia kwenye programu hiyo itakuletea machagua mbalimbali yanayoendana na picha hiyo ikiwemo kama iliwahi kutumiwa katika tukio lingine au watu.

Baada ya hapo utaweza kupata taarifa za msingi ambazo zitakusaidia kujua ukweli wa picha hiyo. Wakati mwingine watu hukua picha na kuweka katika matukio yasiyo halisi ili kupotosha. Lakini programu hiyo itakusaidia kung’amua ukweli matumizi ya picha husika kuhusu Corona. 

Namna nyingine ya kutambua picha za uzushi kupitia yandex ni kupitia program za viunganishi (extension).

Ili uweze kutumia Yandex kwenye program hizo baada ya kuwa nazo kwenye kompyuta , unatakiwa kwenda kwenye habari picha kisha bonyeza upande wa kulia (right click) wa kipanya (mouse) cha kompyuta yako baada ya hapo atakutana na machaguo zaidi ya manne ya jinsi ya kuthibitisha habari picha hiyo.

Machaguo hayo ni Google search, RevEye Search , Bing Image Match, Yandex Search na Baid Search ambapo hutumika katika uthibitishaji habari.

Chagua Yandex  ili kupata majibu ya picha husika na utaweza kufahamu kama habari hiyo ina potosha. Programu hiyo inawafaa wathibitishaji wa habari wa kiwemo wanahabari.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW