“Show” ya kibabe iliyowakutanisha mastaa wa Afrika

Herimina Mkude 0700Hrs   Machi 25, 2022 Burudani
  • Ni show ya Young, Famous & African’ iliyopo Netflix.
  • ‘show’ hii inawahusu nyota maarufu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.
  • Imejaa visa vya mapenzi, chuki na urafiki.

Dar es Salaam. ‘Young, Famous & African’ au kwa kifupi unaweza kuita YFA, ni ‘reality show’ yaani imebeba uhalisia wa maisha ya wahusika.

Natumaini katika pita pita zako kwenye mitandao ya kijamii, umeshakutana na jina hilo.

Wahusika wake ni vijana nyota, maarufu na wenye ‘mishiko’ yao haswaa kutoka nchi mbalimbali Afrika.

Ndani humo utakutana na ‘Dj’ maarufu kusini mwa Afrika, hapa namzungumzia Dj Naked, muimbaji Nadia, mtangazaji maarufu Afrika Kusini Andile, nyota wa muziki kutoka Nigeria 2baba na wengineo.

Bila kuwasahau Zari na Diamond, ambao tunaweza sema wamesababisha Watanzania wengi kuitazama show hiyo.

Nyota hawa ni marafiki na wanajikuta wakikutana kwenye party iliyoandaliwa na muigizaji mrembo Khanyi huko jijini Johannesburg Afrika ya Kusini.

Kukutana kwao kunaanzisha vitu vingi, ikiwemo mapenzi, ugomvi wa hapa na pale, urafiki na mambo mengine.

Visa ni vingi vya kusimulia kutoka kwenye show hii, lakini ningependa tuwaangazie wale ambao wamefanya Watanzania tukajazane huko mjini Netflix.

Hapa nawazungumzia Zari na Diamond.

Nyota hawa wanakutana Afrika Kusini kwenye 'party' walioalikwa na muigizaji maarufu Khanyi. Picha| News24

Kwa upande wa Diamond, kwenye ‘show’ hii amekuwa ni rafiki wa kila mtu kwenye kundi hilo, huku ukaribu anaoujenga na Nadia ukileta sintofahamu kwa wengine.

Zari yeye amekuwa ni mtu wa kugombana na kila mtu kwenye kikundi hiki, mwanzo ilikua na Annie baadaye ukahamia kwa Khanyi ambae walau alikua ‘shosti’.

Hali hiyo inasababisha mwanamama huyu kujikuta kama adui wa wanawake wote kwenye kundi hili hadi kufika chochote atakachokisema lazima kipingwe au kikosolewe.

Licha ya kuwa kila mtu anamchukia Zari, kwa Andile hali ni tofauti, kwani kila amuonapo Zari anatamani watu wote duniani watoweke na wabaki wawili tu.

Kiufupi tunaweza sema Andile amezama kwenye huba kiasi cha kutoona wala kusikia chochote, kinachobaki ni kuwa huba hii itamfikisha wapi wakati mwanamke aliyemzimikia ni mama watoto wa rafiki yake.


Zinazohusiana:


Mwanzo wa sintofahamu

Mambo yanakuwa mambo siku pale ambapo Annie anamwambia Zari kwamba kutokana na kugombana kwao mara kwa mara basi hataki kumuona kwenye harusi yake na 2baba.

Kwa Zari haoni kama kuna kitu amepoteza, kwani yeye na Annie sio marafiki sana.

Kutokuwepo kwa Zari kwenye harusi hiyo ilikuwa ni amani kwa kila mtu ila kwa kijana Andile ulikuwa ni upweke usiopimika, kiasi cha kumfanya ashindwe kukaa hadi mwisho wa sherehe na kuongoza njia hadi nyumbani kwa Zari.

 Andile afikapo kwa Zari anashangaa mbona kama Zari hana amani vile juu ya ujio wake.

Wakati akijiuliza, ghafla Diamond anatokea kutoka chumbani, Andile anashikwa na mshangao na hajui nini cha kufanya huku wivu ukimshika haswaa.

Kijana huyu anajua kwamba Zari na Diamond wana watoto lakini hawana mahusiano yeyote kwa sasa, lakini inakuaje Diamond yupo kwa Zari tena katikati ya usiku?

Sitaki kukumalizia uhondo wote, kaitazame filamu hii ambayo ina ‘trend’ huko mjini Netflix na kiukweli hutojutia muda na  bando lako.

                               

Related Post