Jumatatu, Julai 08, 2024
Dar es Salaam. Wataalamu wa afya na viongozi mbalimbali wameendelea kusisitiza juu ya matumizi ya barakoa kama mojawapo ya njia ya kupambana na ugonjwa wa Corona.
Kati ya barakoa zinazoshauriwa ni pamoja na zile zilizotengenezwa kwa kitambaa ili kupunguza gharama na ulazima wa kununua mara kwa mara barakoa ambazo hazidumu muda mrefu.
Hata hivyo, siyo kila kitambaa kinafaa kutumika kama malighafi ya kutengeneza barakoa. Uzingatie nini ili upate barakoa sahihi? Tazama video hii kufahamu zaidi.