Shule 10 bora matokeo darasa la saba 2020 hizi hapa

Mwandishi Wetu 0538Hrs   Novemba 21, 2020 Habari
  • Kati ya shule 10 bora mwaka huu, nane zinatokea Kanda ya Ziwa.
  • God’s Bridge ya Mbeya yaingia 10 bora na kuzitesa za mwaka jana.

Dar es Salaam. Iwapo ulikuwa ukisubiri kwa hamu kufahamu shule 10 bora katika mtihani wa darasa la saba, hatimaye kitendawili Kimeteguliwa baada ya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kuitangaza Shule ya Msingi God’s Bridge kuwa ndiyo shule bora kitaifa baada ya kushika nafasi ya kwanza.  

Shule hiyo iliyopo mkoani Mbeya imeipiku Shule ya Msingi Graiyaki ya mkoani Mara iliyokuwa imeshika nafasi ya kwanza katika matokeo ya mtihani ya darasa la saba mwaka 2019.

 Katika matokeo ya mwaka huu Graiyaki imeporomoka hadi nafasi ya tano.

God’s Brigde, ambayo haikuwepo katika shule 10 bora mwaka jana, katika matokeo ya mwaka huu imefuatiwa kwa karibu na Bunazi Green Acres ya mkoani Kagera pamoja na Twibhoki ambayo imeendelea kung’ang’ania katika orodha hiyo ya juu.


Soma zaidi: 


Shule nyingine zilizofanikiwa kuingia kwenye 10 bora katika matokeo ya mwaka 2020 yaliyotangazwa leo na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde jijini Dar es Salaam ni Kwema Modern ya Shinyanga, Kemebos na Rweikiza za Kagera, St Anne Marie (Dar es Salaam), Mumtaaz (Mwanza) na Rocken Hill ya Shinyanga.

Kati ya shule 10 zilizoingia katika orodha hiyo ya dhahabu, nane zinatokea Kanda ya Ziwa na kuifanya kanda hiyo kuendelea kutawala katika matokeo hayo ya darasa la saba.

Shule tisa kati ya 10 zilizotangazwa katika 10 bora zilikuwa na madarasa yenye wanafunzi wasiozidi 100 kasoro Shule ya St Anne Marie pekee iliyokuwa na wanafunzi 129 ambao ni takriban mara tatu ya wanafunzi waliokuwepo God’s Bridge.

Shule hiyo ya God’s Bridge iliyoongoza kitaifa ilikuwa na wanafunzi 47 pekee kwa mujibu wa NECTA. 

Kupata matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2020 ingia hapa

Related Post