Siyo kweli wananchi Italia wanatupa pesa mitaani kuepuka Corona

Daniel Mwingira 0303Hrs   Aprili 02, 2020 NuktaFakti
  • Picha zinazosambaa mtandaoni ni za fedha zilizoisha muda wake katika nchi ya Venezuela ambayo ilibadilisha noti zake mwaka 2018.
  • Picha hizo ni uzushi unaolenga kuibua taharuki ya Corona. 

Dar es salaam. Ugonjwa wa virusi vya Corona umeendelea kushika kasi duniani na kuleta madhara makubwa katika nchini mbalimbali ikiwemo kudorora kwa shughuli za uzalishaji bidhaa na utoaji huduma muhimu kwa ajili ya maendeleo. 

Janga hilo pia limekuwa ni fursa kwa baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii kupotosha kuhusu taarifa za matukio ya mlipuko wa ugonjwa huo, jambo linalozidisha athari za kisaikolojia kwa watu. 

Kumekuwa na picha ambazo zimeanza kusambaa tangi Machi 31, 2020 zikionyesha kiasi kikubwa cha pesa zilizozagaa mitaani na baadhi ya watu wamehusisha picha hizo na athari za Corona katika nchi ya Italia ambayo sasa inaongozwa kwa watu wengi waliofariki kutokana na ugonjwa huo.  

 

Picha hizi mbili zimewekewa maneno yanayosema  "Please take COVID-19 seriously. People in Italy are throwing away their money in the streets because they feel that money can not help them anymore!

Tasfri yake ikiwa 'Tafadhali kuwa makini na ungojwa wa corona (COVID-19 ). Nchini Italia watu wanatupa hela zao mitaani wakifikiri kuwa pesa haziwezi kuwasaidia tena.

Lakini habari  hiyo ni ya uzushi.


Soma zaidi: 



Huu ndiyo ukweli

Utafiti wa kihabari uliofanywa na tovuti ya habari ya www.nukta.co.tz  umebaini kuwa picha hizo hazihusiani na yanayoendelea nchini Italia kwa sasa na ni uzushi wa baadhi ya watu kuibua taharuki juu ya ugonjwa wa Corona. 

Kwa tumia zana za kidijitali, Nukta imebaini kuwa picha hizo ni za habari  kutoka  nchi ya Venezuela na zilichapishwa Machi 12, 2019 na tovuti ya Maduradas ya Venezuela ambayo inaonyesha fedha ambazo zimetawanyika mtaani nchini humo. 

Fedha hizo za zamani zilizagaa mitaani kwa sababu nchi hiyo ilibadilisha noti zake mwaka 2018 na fedha nyingi zikabaki bila thamani. 

Hata hivyo, polisi wa nchi hiyo ambayo haina utulivu wa kisiasa, walizikusanya na kuzichoma moto ili kuondoa usumbufu kwa wananchi. 

Fedha zilizoisha muda wa matumizi yake zilizozagaa katika mitaa mbalimbali ya Venezuela zikichomwa moto. Picha| Maduradas.

Related Post