Jeshi la Polisi lamsaka aliyehusika na mauaji katika sherehe ya ‘birthday’ Mwanza

Mariam John 0949Hrs   Aprili 09, 2024 Habari
  • Tukio hilo lilitokea Aprili 7 mwaka huu Ustawi-Buzuruga wilayani Ilemela.
  • Jeshi la Polisi laahidi kushirikiana na wananchi kumsaka mtuhumiwa.

Mwanza.Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linamsaka kijana mmoja anayefahamika kwa jina la David Deogratius kwa kuhusika na mauaji ya Peter John (19) yaliyofanyika katika sherehe ya kuzaliwa (birthday party) Ustawi-Buzuruga wilayani Ilemela.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Wilbrod Mutafungwa amewaambia wanahabari kuwa tayari jeshi hilo limeanza kumsaka muhusika ili aweze kuchukuliwa hatua.

“Jeshi la Polisi tukishirikiana na wananchi tunaendelea na msako kuhakikisha kijanan huyo aliyehusika na mauaji anakamatwa na anachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria,” amesema Mutafungwa leo Aprili 9,2024.

Chanzo chabainika

Mutafungwa amewaambia wanahabari kuwa tukio hilo lilitokea April 7 mwaka huu saa 5: 00 usiku ambapo marehemu alifika kwenye mji wa Osombo Osombo ambako kulikuwa na sherehe za kuzaliwa mtoto huyo.

Amesema wakiwa wanaendelea kusherehekea kwa kumwagiana maji kama ishara za kusherehekea siku hiyo, ulizuka ugomvi kati ya marehemu na mtuhumiwa David Deogratius ambapo alimshambulia mwezake kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali karibu na kifua na kuanguka chini.

“Wakati sherehe hizo zikiendelea katika familia hiyo kuliibuka ugomvi kati ya David Deogratius na Yohana John ndipo David alimshambulia mwenzake kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali na kumjeruhi kifuani na baada ya tukio hilo mtuhumiwa alitoweka mara baada ya kuona mwenzake ameaguka chini,” amesema Kamanda Mutafungwa.


Soma zaidi:Sera 4 kukuza uchumi, usawa Afrika


Baada ya tukio hilo David Deogratius alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekou-Toure.

Aidha, Mutafungwa ameutaarifu umma kuhusu tukio lingine la mtu mmoja aliyekuwa akifanya kazi za ujenzi katika bandari ya Mwanza kaskazini, Riziwani Songora(45) aliyefariki  dunia baada ya kutumbukia kwenye maji katika Ziwa Victoria wakati akiwa anafanya kazi za ujenzi wa ghati katika bandari hiyo.

“Tukio hilo ni ajali, na kama tunavyofahamu katika mkoa wetu wa Mwanza kuna shughuli za ujenzi wa bandari kwa ajili ya maegesho ya meli mpya ya Mv Mwanza, sasa wakati marehemu akiendelea na shughuli hiyo alitumbukia ziwani,” amesema Mutafungwa.

Kamanda huyo amesema kuwa  juhudi za uokozi zilifanyika lakini alifariki dunia wakati anakimbizwa katika hospitali ya Bugando kwa ajili ya matibabu.

Related Post