Mwigulu azindua kituo cha uokoaji Mwanza, asisitiza uwajibikaji

January 23, 2026 6:17 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Kituo hicho kitaendeshwa kwa saa 24 ili kuhakikisha usalama wa wananchi na wasafiri wanaotumia Ziwa Victoria unalindwa wakati wote.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Tanzania Dk Mwigulu Nchemba amewaagiza watendaji wa kituo cha kisasa cha utafutaji na uokoaji majini kilichopo jijini Mwanza kutumia vizuri kituo hicho kuokoa maisha ya Watanzania wanaotumia Ziwa Victoria.

Dk Nchemba ametoa maagizo hayo leo Januari 23, 2026, baada ya kutembelea kituo hicho akisisitiza kuwa uzembe wowote utakaotokea wakati wa uokoaji inapotokea ajali ziwani wahusika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

“Huduma za uokozi ni kazi ya kuokoa maisha, hivyo hakuna uvumilivu kwa uzembe, kuchelewesha utoaji wa huduma za msaada pindi inapohitajika,” amesisitiza Dk Mwigulu.

Kituo hicho ambacho ni cha kwanza nchini kimejengwa kutokana na changamoto za ajali majini zilizokuwa zikijitokeza katika Ziwa Victoria, ambapo takriban watu 20 wamepoteza maisha katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Miongoni mwa ajali hizo zilizosababisha upotevu wa maisha ya Watanzania ni ajali ya ndege kampuni ya Precision Air iliyotokea Novemba 6, 2022 na kusababisha vifo vya watu 19 na majeruhi 26.

Dk Mwigulu amefafanua kuwa licha umuhimu wa kituo hicho kilichotumia Sh19.8 bilioni kukamilika, ujenzi wake ulisimama kwa miaka miwili kati ya mwaka 2018 hadi 2020 baada ya wahisani kujiondoa.

Aidha, Dk Mwigulu ameagiza kituo hicho kuendeshwa kwa saa 24 ili kuhakikisha usalama wa wananchi na wasafiri wanaotumia Ziwa Victoria unalindwa wakati wote.

“Ikitokea mtu akapigiwa simu ya dharura, ikatokea amesinzia, mtu wa aina hiyo mheshimiwa Waziri wala usimuamishe kituo, fukuza kabisa…kwa sababu hii ni kazi inayotaka mtu azingatie na atoe msaada kwa wakati ule msaada unaotakiwa,” amesisitiza Dk Mwiguru.

Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema mbali na makao makuu ya kituo hicho kuwa jijini Mwanza, Serikali imejenga vituo vingine vitatu Musoma, Ukerewe na eneo lingine la Ziwa Victoria ili kuhakikisha usalama wa watumiaji majini.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
28 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
28 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
28 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Jinsi afya ya akili inavyowatesa wanawake makazini

Jinsi afya ya akili inavyowatesa wanawake makazini

Nukta TV

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV