Mtoto 1 kati ya 3 duniani ndiye anayeweza kusoma na kuelewa hadithi fupi

September 17, 2022 9:41 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Mkutano wa Ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa elimu duniani ukianza leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limetoa taarifa inayoeleza idadi ya Watoto wasiojua kusoma imeongezeka ulimwenguni ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita. 

Kabla ya Janga la COVID-19 miaka miwili iliyopita watoto waliojua kusoma wenye umri wa miaka 10 ulimwenguni walikuwa nusu lakini sasa UNICEF linasema idadi yao ni theluthi moja hii ikiwa sawa na mtoto mmoja kati ya watatu ndio mwenye uwezo wa kusoma na kuelewa hadithi fupi.

“Shule hazina rasilimali, walimu wanalipwa ujira mdogo, walimu wengine wasio na sifa wanaajiriwa, msongamano wa wanafunzi madarasani, mitaala ya kizamani na vyote hivi vinasababisha Watoto kushindwa kufikia uwezo wa juu wa ufaulu.” amesema  Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell katika taarifa yake iliyotolewa jijini New York Marekani jana Septemba 16.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Nukta TV

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Nukta TV

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Nukta TV