Ni haki yao: Watoto wenye ulemavu wapewe maisha, elimu bora

November 11, 2021 6:12 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Mtoto mlemavu 1 kati ya 10 anakosa mahitaji ya msingi ikiwemo afya.
  • Watakiwa kujumuishwa kwenye jamii kama watoto wengine.
  • Serikali zatakiwa kuweka mikakati kuwainua kimaisha.

Ripoti mpya shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto (UNICEF) imeeleza kuwa mtoto mlemavu 1 kati ya 10 anakosa mahitaji ya msingi ikiwemo afya, elimu na ulinzi, jambo linaloibua matabaka baina yao na watoto wengine. 

Ripoti hiyo hiyo ya hali ya watoto duniani kwa mwaka 2021 iliyozinduliwa Novemba 10 jijini New York, Marekani  imebainisha kuwa idadi ya watoto wenye ulemavu duniani inakadiriwa kuwa takribani milioni 240.

Imebaini kuwa watoto wenye ulemavu wanakosa fursa ikilinganishwa na watoto wasio na ulemavu katika hatua nyingi za ustawi na makuzi, iambapo mtoto mmoja kati ya 10 anakosa mahitaji ya msingi ikiwemo afya, elimu na ulinzi. 

“Utafiti huu mpya unathibitisha kile ambacho tayari tunakifahamu kuwa watoto wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto kubwa na mara nyingi athari limbikizi katika kutekeleza haki zao,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Henrietta Fore. 

“Ikiwa ni kuhusu upatikanaji wa elimu au vitabu ambavyo wale walio karibu nao wangeweza kuwasomea nyumbani, watoto wenye ulemavu mara nyingi hawajumuishwi au kusikika katika karibu maeneo yote yaliyotathminiwa. watoto hawa mara nyingi huachwa nyuma.” 

Ripoti hiyo inajumuisha takwimu kutoka nchi 42 na inashughulikia zaidi ya viashiria 60 vya ustawi wa watoto.  Mwalimu Mary Kaluzi wa Shule ya Msingi Twiga iliyopo katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam akifuatilia namna wanafunzi wake wenye uziwi wanavyojibu maswali darasani hivi karibuni. Picha| Zahara Tunda.

Ripoti pia inaangazia kwa uwazi vikwazo vinavyozuia watoto wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika jamii na athari mbaya za kiafya na kijamii ambazo mara nyingi hutokea.

Hata hivyo UNICEF imesema , uzoefu wa ulemavu unatofautiana sana. Utafiti unaonyesha kuwa hatari na hali hutofautiana kulingana na aina ya ulemavu, mahali ambapo mtoto anaishi na huduma ambazo anaweza kufaidika nazo. 

Waandishi wa ripoti hiyo wanaona kuwa watoto ambao wana matatizo ya kuwasiliana na kujitunza ndiyo wanao uwezekano mkubwa wa kuwa nje ya shule, bila kujali kiwango cha elimu kinachozingatiwa.  

Viwango vya Watoto kuwa nje ya shule ni vya juu kati ya watoto wenye ulemavu wa aina nyingi, na tofauti huongezeka wakati kiwango cha ulemavu kinapozingatiwa.

“Elimu jumuishi haiwezi kuonekana kuwa ni anasa bali ni haki. Kwa muda mrefu sana, watoto wenye ulemavu wametengwa na jamii , lakini hakuna mtoto anayepaswa kutengwa. Uzoefu wangu mwenyewe kama mwanamke kijana mwenye ulemavu unathibitisha uchunguzi huu,” ameeleza Maria Alexandrova (20), mwanaharakati kijana wa UNICEF ambaye anatetea elimu jumuishi  kutoka Bulgaria. 

UNICEF inatoa wito kwa serikali kuwapa watoto wenye ulemavu fursa sawa na wengine, kuondoa vikwazo vya kimwili, kifedha, na kimiundombinu vinavyowasababishwa wakaachwa nyuma katika jamii. 

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW