Mkopo wa Sh53.09 bilioni ulivyokwamisha miradi ya maendeleo Wizara ya Madini

April 27, 2026 4:09 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Kamati yatajwa kutokuridhishwa na upataikanaji wa fedha hizo.
  • Yataka Serikali kupunguza utegemezi wa mikopo ya nje.

Dar es Salaam. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imebaini ucheleweshaji mkubwa wa fedha za miradi ya maendeleo katika Wizara ya Madini, ikichangiwa na kukosekana kwa mikopo kutoka kwa wadau wa maendeleo.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Simon Songe, aliyekuwa akiwasilisha maoni ya kamati yake bungeni Dodoma leo Aprili 27,2026 amesema kukosekana kwa mkopo wa Sh53.09 bilioni kutoka Serikali ya Hispania katika mwaka wa fedha 2025/2026 kulikwamisha utekelezaji wa baadhi ya miradi.

”Mapokezi hafifu ya fedha za maendeleo yanatokana na kutokupatikana kwa mkopo wa Sh53.09 bilioni ambao ulikuwa unatoka Serikali ya spain(Hispania) mkopo huu ulilengwa kutumiwa na taasisi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili kutekeleza mradi wa utafiti wa madini nchini,” inaeleza taarifa ya kamati.

GST ni taasisi ya utafiti chini ya Wizara ya Madini na ilianzishwa baada ya Marekebisho ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. Taasisi hiyo inatekeleza miradi ya utafiti wa madini na nishati kama dhahabu, kinywe na jotoardhi ili kubaini maeneo yenye rasilimali kwa ajili ya uwekezaji.

Kwa mwaka wa fedha 2025/2026, wizara hiyo iliidhinishiwa jumla ya Sh124.6 bilioni sawa na asilimia 55.38 ya bajeti yote kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ikiwemo zinazotekelezwa na GST.

Hadi kufikia Februari 2026, Wizara ya Madini ilikuwa imepokea asilimia nane tu ya bajeti ya maendeleo, hatua inayotafsiriwa kuwa pengo kubwa la utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika sekta hiyo.

“ Upungufu huu wa bajeti unaathiri kwa kiasi kikubwa utekelezaji na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo ambayo ilipangwa kutekelezwa na wizara ya madini,” anaeleza Songwe aliyekuwa akiwasilisha mapendekezo kamati.

Ucheleweshaji wa fedha za maendeleo umekuwa miongoni mwa changamoto  inayozikabili wizara nyingi nchini ikichangiwa kwa kiasi kikubwa na utegemezi wa mikopo na misaada kutoka nje. 

Changamoto hiyo imekuwa ikiathiri kasi ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika sekta mbalimbali, ikiwemo sekta ya madini.

Ili kutatua changamoto hiyo, kamati imeishauri Serikali kuhakikisha inatenga fedha za ndani kwa kipaumbele katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kupunguza utegemezi wa mikopo ya nje ambayo imekuwa ikichelewesha utekelezaji wa miradi muhimu.

Kwa mwaka wa fedha 2026/27 wizara hiyo imeomba kuidhinishiwa bajeti hiyo Sh174.98 bilioni iliyoongezeka kwa asilimia 22 kulinganisha na ile iliyoidhinishwa mwaka uliopita.

Sh71.50 imetengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo ikipungua kwa asilimia 14.49 kutoka Sh124.60 bilioni iliyotengwa mwaka uliopita,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI, WIZARA YA MADINI IKIWASILISHWA BUNGENI

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI, WIZARA YA MADINI IKIWASILISHWA BUNGENI

Nukta TV

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Nukta Africa kuzindua Nukta AI, siku ya uhuru wa vyombo vya habari

Nukta Africa kuzindua Nukta AI, siku ya uhuru wa vyombo vya habari

Nukta TV