Mgonjwa wa kwanza afariki dunia kwa corona Tanzania

March 31, 2020 10:19 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Amefariki leo asubuhi katika kituo cha matibabu cha wagonjwa wa COVID-19 kilichopo Mloganzila jijini Dar es Salaam.
  • Marehemu ni Mtanzania, mwanaume mwenye umri wa miaka 49 ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine.
  • Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu awataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari. 

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imetangaza kifo cha kwanza cha mgonjwa wa virusi vya Corona kilichotokea alfajiri ya leo ( Machi 31, 2020) jijini Dar es Salaam. 

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  leo inaeleza kuwa mgonjwa huyo amefariki katika kituo cha matibabu cha wagonjwa wa COVID-19 kilichopo Mloganzila jijini Dar es Salaam. 

Amesema marehemu huyo ni Mtanzania, mwanaume mwenye umri wa miaka 49 ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine.

Hadi kufikia leo, Tanzania imethibitisha kuwa na wagonjwa 19 wa virusi hivyo vinavyosambaa kwa kasi duniani ambapo mgonjwa mmoja kati ya hao tayari amepona. 

Mkoa wa Dar es Salaam  ndiyo unaongoza kuwa na wagonjwa wengi wa Corona wanaofikia 11 ukifuatiwa na visiwa vya Zanzibar (5), Arusha (2) na mmoja alithibitishwa katika mkoa wa Kagera.

“Kazi ya kufuatilia watu waliokutana na wagonjwa hawa inaendelea (contact tracing). Aidha tunawataka wananchi wote waendelee kuchukua tahadhari kujikinga na ugonjwa huu,” alisema Ummy jana wakati akitangaza wagonjwa wengine watano wa Corona.


Zinazohusiana


Tahadhari ambazo zinatakiwa kuchukuliwa ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara, kutokugusa macho, pua au mdomo, kutumia tishu wakati wa kukohoa na kuepuka mikusanyiko ya watu isiyo ya lazima.

Mpaka sasa ni nchi nne za Afrika Mashariki za Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda ndiyo zimethibitisha kuwa na wagonjwa wa vurusi hivyo na vifo vya watu wawili wa ugonjwa vilivyotokea Kenya na Tanzania.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV