BoT yabakiza riba ya benki kuu 5.75% licha ya vita Mashariki ya Kati

April 1, 2026 2:46 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Yaeleza kuwa viashiria vya kiuchumi vinaonyesha kuwa vipo imara kiasi cha kutoathiriwa vibaya sana na  athari ya vita kati ya Marekani na Israel dhini ya Iran.

Dar es Salaam. Kamati ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeendelea kubakiza riba ya benki kuu (CBR) kuwa asilimia 5.75 katika robo ya pili ya mwaka 2026 kudhibiti mfumuko wa bei licha ya athari ya vita inayoendelea Mashariki ya Kati kutishia ukuaji wa uchumi nchini. 

Hii ni mara ya tatu mfululizo kamati hiyo inabakiza kiwango hicho cha riba ambacho BoT hutumia katika kufanya biashara na benki za biashara. 

Hata hivyo, safari hii mazingira ni tofauti kidogo kutokana na kuwepo kwa vita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran ambayo imesababisha kupaa kwa bei ya mafuta ya petroli na kuathiri mnyororo mzima wa ugavi wa huduma na bidhaa ulimwenguni.

Vita hiyo, yenye zaidi ya mwezi mmoja, imesababisha kushambuliwa kwa visima vya mafuta, maghala ya kuhifadhi mafuta na viwanda vya kusafisha mafuta (refineries) pamoja na Irani kufunga lango la Hormuz linalopitisha takriban asilimia 20 ya mafuta yanayosafirishwa kwenda katika masoko mbalimbali duniani. 

Katika mkutano wake na wanahabari na mabosi wa benki na kampuni za simu, Naibu Gavana wa Sera za Uchumi na Fedha wa BoT, Dk Yamungu Kayandabila amesema kuwa uamuzi wa kuacha riba hiyo katika kiwango cha asilimia 5.75 umetokana na kuwepo viashiria chanya vya ukuaji wa uchumi licha ya athari za vita inayoendelea. 

Dk Kayandabila amesema mfumuko wa bei katika robo ya kwanza ya mwaka ulikuwa imara ndani ya wastani wa asilimia 3.3 Tanzania Bara na asilimia 4.5 kwa Zanzibar, vikichangiwa na sera imara za fedha na uhimilivu wa bei za vyakula na nishati. 

Vita ya Iran tishio ukuaji wa uchumi Tanzania

“MPC inatarajia mfumuko wa bei kuendelea kuwa ndani ya wigo wa asilimia 3 hadi 5 katika robo ya pili huku presha ya kuongezeka kwa bei ya nishati na usafiri ikitegemewa kupunguzwa kasi na gharama za chini za vyakula na uimara wa Shilingi,” amesema kigogo huyo wa BoT jijini Dar es Salaam. 

Kamati hiyo imebakiza kiwango hicho wakati tayari Watanzania wameshaanza kuonja maumivu ya kupanda kwa gharama za mafuta Aprili Mosi kufikia Sh3,820 kwa lita ya petroli, sawa na ongezeko la asilimia 33 ndani ya mwezi mmoja kutokana na athari ya vita kati ya Marekani na Israel dhini ya Iran. 

Katika robo ya pili inayoanzia Aprili hadi Juni 2026, BoT inatarajia kuwa uchumi utaendelea kuwa imara na kufikia ukuaji wa asilimia 6.1 kwa Tanzania Bara na asilimia 6.6 kwa upande wa visiwani Zanzibar. 

“Hata hivyo, kuendelea au kuchochewa zaidi kwa mgogoro Mashariki ya Kati kunaweza kuathiri mwenendo wa ukuaji wa uchumi siku zijazo,” amesema Dk Kayandabila.

Kamati ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema imebaini kuwa mgogoro unaoendelea Mashariki ya kati unaweza kuwa na athari kubwa katika uchumi wa Tanzania.

Mgogoro huo, wenye zaidi ya mwezi mmoja, umesababisha kushambuliwa kwa visima vya mafuta, maghala ya kuhifadhi mafuta na viwanda vya kusafisha mafuta (refineries) pamoja na Irani kufunga lango la Hormuz linalopitisha takriban asilimia 20 ya mafuta yanayosafirishwa kwenda katika masoko mbalimbali duniani. 

Katika mkutano wake na wanahabari na mabosi wa benki na kampuni za simu, Naibu Gavana wa Sera za Uchumi na Fedha wa BoT, Dk Yamungu Kayandabila amesema kuwa hata hivyo ukuwaji wa uchumi nchini  umeendelea kuwa thabiti ambapo katika robo ya kwanza mwaka huu, ambapo uchumi wa Tanzania Bara unakadiliwa kufikia asilimia 6.2 na asilimia 6.7 kwa upande wa Zanzibar. 

Dk Kayandabila amesema katika robo ya pili inayoanzia Aprili hadi Juni 2026, BoT inatarajia kuwa uchumi utaendelea kuwa imara na kufikia ukuaji wa asilimia 6.1 kwa Tanzania Bara na asilimia 6.6 kwa upande wa visiwani Zanzibar. 

Pia MPC inatarajia mfumuko wa bei kuendelea kuwa ndani ya wigo wa asilimia 3 hadi 5 katika robo ya pili huku presha ya kuongezeka kwa bei ya nishati na usafiri ikitegemewa kupunguzwa kasi na gharama za chini za vyakula na uimara wa Shilingi,” amesema kigogo huyo wa BoT jijini Dar es Salaam. 

Kamati hiyo imebakiza kiwango hicho wakati tayari Watanzania wameshaanza kuonja maumivu ya kupanda kwa gharama za mafuta Aprili Mosi kufikia Sh3,820 kwa lita ya petroli, sawa na ongezeko la asilimia 33 ndani ya mwezi mmoja kutokana na athari ya vita kati ya Marekani na Israel dhini ya Iran. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW