Vodacom Tanzania yamwaga Sh70 bilioni kuboresha M-Pesa

April 2, 2026 2:56 pm ยท Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwa wateja na kukimbizana na kasi ya uchumi wa kidijitali.

Dar es Salaam. Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imewekezaย  Dola za Marekani milioni 28 (zaidi ya Sh70 bilioni) kuboresha huduma za kifedha kwa njia ya simu ya M-Pesa ikiwa ni jitihada za kuendana na mahitaji ya soko ya uchumi wa kidijiti.ย ย 

Katika maboresho hayo, Vodacom imebadili mfumo wa zamani wa M-Pesa unaofahamika kama G2 kwenda mfumo mpya wa Fintech 2.0 unaolenga kutatua changamoto na kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja.

Mabadiliko hayo ya kiteknolojia yamefanyika usiku wa kuamkia leo Aprili 2, 2026 kuanzia saa sita usiku hadi saa 10 alfajiri, ambapo kwa muda huo huduma za M-Pesa zilisitishwa kupisha uhamishaji wa mfumo.

M-Pesa ni moja ya huduma za kifedha zinazotumiwa na mamilioni ya watu nchini. Kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) hadi Desemba 2025 M-Pesa ilikuwa inaongeza kwa watumiaji ikiwa na akaunti 31,488,157 sawa na asilimia 41.17 ya akaunti zote zilizohai.ย 

Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni amesema maboresho hayo ni kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwa wateja na kukimbizana na kasi ya uchumi wa kidijitali. Picha | Kitomari Banking and Finance Blog.

Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni, aliwaambia wanahabari jijini Dar es Salaam Aprili Mosi, 2026 kuwa mabadiliko hayo yanalenga kuendana na mageuzi ya mahitaji ya soko na kuboresha huduma za kifedha kwa watumiaji.

โ€œTunahitaji kwenda kwenye teknolojia ya juu zaidiโ€ฆ tumetoka kwenye huduma za miamala tumekwenda kwenye huduma za kifedha,โ€ amesema Mbeteni.

Mbeteni ameongeza kuwa mabadiliko hayo yanaenda sambamba na mwelekeo wa Taifa linalokimbia kwa kasi kwenye uchumi wa kidijitali likiwa na zaidi ya watumiaji milioni 76 wa huduma za kifedha kwa njia ya simu. Idadi hiyo ya watumiaji wa huduma za kifedha, amesema, inatarajiwa kuongezeka mara mbili ifikapo 2050.ย 

Kukwama kwa huduma sasa basi

Maboresho hayo ya M-Pesa yataisaidia kampuni hiyo iliyoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kuwapatia wateja wao maboresho ya huduma wakati wa changamoto bila ya kusitishwa kwa muda (outage) hususan nyakati za usiku au alfajiri.

Utetelekaji wa mtandao au mfumo wa huduma za kifedha huathiri watumiaji wakiwemo wafanyabiashara wadogo wanaotegemea teknolojia hiyo kupata mikopo, kupokea malipo na kununua bidhaa mbalimbali ndani na nje ya nchi.ย 

Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia cha M-Pesa, Athumani Mlinga, amesema kwa sasa mteja anaweza kuendelea kutuma au kupokea fedha hata wakati mfumo unafanyiwa marekebisho hatua inayotarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa usumbufu uliokuwa ukijitokeza hapo awali.

Athumani Mlinga, amesema kwa sasa mteja anaweza kuendelea kutuma au kupokea fedha hata wakati mfumo unafanyiwa marekebisho. Picha | Swahili Times

Mfumo huo mpya una uwezo wa kuchakata zaidi ya miamala 1,000 kwa sekunde kulinganisha na mfumo wa zamani uliokuwa ukichakata miamala 800, hatua itakayopunguza ucheleweshaji wa miamala wakati wa mahitaji makubwa.

โ€œHata kama kampuni nyingine zitasitisha huduma za kifedha kupitia simu za mkononi, M-Pesa ina uwezo wa kuhudumia โ€˜populationโ€™ ya watumiaji wote nchini,โ€ amesema Mlinga.

Mweleko chanya kuelekea uchumi wa kidijiti

Hii ni mara ya kwanza kwa Vodacom Tanzania kufanya maboresho makubwa ya mfumo wa M-Pesa tangu ilipofanya hivyo miaka tisa iliyopita huku uwekezaji huo ukigharimu takriban Sh70 bilioni katika mradi huu uliodumu kwa miezi 18.

Kwa M-pesa ambayo ina zaidi ya namba za malipo (Lipa Namba) 600,000 nchi nzima, hatua hii inaweza kuongeza ujumuishaji wa kifedha, kupunguza utegemezi wa fedha taslimu na kuwezesha biashara ndogo na za kati kushiriki kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa kidijitali.

Aidha, Vodacom imeainisha kuwa imeweka kipindi maalum cha siku 30 za huduma mahususi kwa Wateja (HyperCare), ambapo timu za kiufundi na huduma kwa wateja zitafanya kazi kwa karibu zikifuatilia na kushughulikia changamoto zozote zitakazojitokeza kutokana na mabadiliko hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW