Mfumuko wa bei wang’ang’ania kiwango cha Oktoba 2024

December 10, 2024 3:08 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Wasalia kuwa asilimia 3 sawa na kiwango kilichorekodiwa Oktoba mwaka huu.

Arusha. Kasi ya mfumuko wa bei ya bidhaa na huduma nchini Tanzania kwa mwaka unaoishia mwezi Novemba 2024 imebakia kuwa asilimia 3 sawa na kiwango kilichorekodiwa mwaka unaoishia Oktoba mwaka huu.

Taarifa ya mwenendo wa mfumuko wa bei nchini iliyotolewa leo Disemba 10, 2024 na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (Nbs)  inabainisha kuwa hali hiyo imechangiwa na kupungua na kuongezeka kwa kwa mfumuko wa bei kwa baadhi ya bidhaa.

“Kasi ya Mfumuko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2024 kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2024 kumechangiwa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa bidhaa za vyakula na kupungua kwa mfumuko wa bei kwa bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2024 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2024” imesema taarifa ya Nbs.

Kwa mujibu wa Nbs hali hiyo inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2024 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2024.

Enable Notifications OK No thanks