Mbaroni kwa kukwepa kodi ya ardhi zaidi ya Sh4.2 bilion

March 19, 2022 10:22 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Wadaiwa hao sugu wanatoka Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana na Ilemela.
  • Wameshindwa kulipa kodi ya ardhi ya zaidi ya Sh4.2 bilioni.

Mwanza. Wadaiwa sugu 400 wa kodi ya ardhi wamefikishwa katika Mahakama ya Ardhi ya Mkoa wa Mwanza kwa kushindwa kulipa kodi ya ardhi ya zaidi ya Sh4.2 bilioni.

Kamishina wa ardhi Mkoa wa Mwanza, Eliah Kamiyanda amesema watu hao ni wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana na Ilemela.

Amesema kwa mujibu wa taratibu za kisheria zipo hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Idara ya Ardhi katika kuwaelimisha na kuwakumbusha  wananchi wajibu wao kulipa kodi ya ardhi ingawa wengi wao hawafanyi hivyo.

“Kutokana na tatizo hilo, kupitia kifungu cha 50 cha Sheria ya Ardhi, mtu yeyote anayekaidi kulipia kodi ya ardhi,  Kamishina ana wajibu wa kuwafikisha mbele ya sheria watu hao ili waweze kujibu mashtaka yao,” amesema Kamiyanda.


Soma zaidi:


Amesema ofisi hiyo inakusanya kodi ya ardhi kwa mujibu wa sheria na kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, iliweza kukusanya zaidi ya Sh8 bilioni  huku watu ambao walikaidi kulipa walifikishwa mahakamani.

“Kama ofisi ya ardhi mwaka huu, tumejiwekea malengo ya kukusanya zaidi ya Sh18 bilioni,” amesema Kamiyanda huku akituma ujumbe kwa walipa kodi katika wilaya zingine za Mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanajitokeza kulipa kodi hizo ambapo wadaiwa katika wilaya hizo wanatakiwa kulipa deni la Sh7 bilioni.

Amebainisha kuwa changamoto zinazowakabili wakusanya kodi kutoka kwenye ofisi hiyo ni pamoja na watu kutokuwa na utayari wa kutekeleza takwa hilo kwa mujibu wa sheria.

Pamoja na changamoto hizo wapo wanaothamini suala hilo na wanalipa kodi kwa hiari yao huku wale ambao hawatii wanachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV