Miili ya wanawake watatu waliouawa yazikwa Mwanza

January 22, 2022 11:14 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni ndugu wa familia moja walikutwa wameuawa kando ya mto mkoani Mwanza.
  • Wazikwa jana Sengerema, polisi wakiendelea na uchunguzi.

Mwanza. Maiti za wanawake watatu waliokutwa wameuawa na kutupwa kando ya mto nyuma ya Kituo cha Afya Buzuruga, mtaa wa Mecco Kusini wiki hii imetambuliwa na ndugu zao na imezikwa jana wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza,Gidion Msuya tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Januari 19, 2022 ambapo miili hiyo ilikutwa na majeraha katika maeneo mbalimbali kando ya mto uliopo nyuma ya kituo hicho cha afya. 

Msuya amesema baada ya kutoa matangazo kuhusu vifo vya wanawake hao ambao awali hawakutambulika, ndugu wamejitokeza na kuwatambua majina yao.

Wanawake hao watatu ni ndugu wa familia moja ambao ni Mary Charles,  Janeth Fred na Monica Jonas.

Kati ya waliouawa mwanamke mmoja Janeth Fred ameacha mtoto mwenye umri wa mwezi mmoja na Monica akiacha mtoto mwenye umri wa miezi sita.

Kwa mujibu wa Msuya, tayari wanawashikilia watu kadhaa kwa mahojiano kutokana na tukio hilo na uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo unaendelea.

Enable Notifications OK No thanks