Maumivu tena bei za mafuta zikipanda Tanzania

August 7, 2024 4:40 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei ya rejareja ya Petroli imeongezeka kwa Sh21 na kufikia Sh3,231 kwa lita wakati dizeli ikiongezeka kwa Sh16 na kufika Sh3,131 kwa lita moja.
  • Ongezeko limechangiwa na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na mabadiliko ya gharama za uagizaji wa bidhaa hiyo.

Dar es Salaam. Wamiliki wa vyombo vya moto nchini watalazimika kujifunga mkanda ili kumudu gharama za mafuta ya petroli na dizeli baada ya bei ya nishati hiyo kuongezeka ndani ya mwezi mmoja ikichagizwa na kuongezeka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia. 

Julai angalau bei za mafuta zilipungua kidogo na kuuzwa Sh3,210 kwa petroli kutoka Sh3,261 Juni mwaka huu wakati dizeli ilipanda kidogo hadi Sh3,115 kwa lita ya dizeli kutoka Sh3,112 kwa lita jijini Dar es Salaam hali iliyowapa ahueni watumiaji wa vyombo vya moto kabla ya kuanza kupanda tena mwezi huu. 

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma kuhusu bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), wakazi wa Dar es Salaam wao watanunua mafuta ya petroli kwa bei ya rejareja ya Sh3,231, ikiwa ni Sh21 zaidi ya bei waliyonunulia Julai mwaka huu. Bei ya mafuta ya dizeli nayo imepanda kwa Sh16 hadi Sh3,131 kwa lita kutoka Sh3,115 iliyorekodiwa Julai.

Hata Hivyo, bei ya mafuta ya taa imeshuka kiduchu kwa Sh4 ambayo kwa sasa yatauzwa kwa Sh3,257 kwa lita kwa bei ya rejareja jijini Dar es Salaam.

Ewura imeeleza kuwa kuongezeka kwa bei za mafuta kumesababishwa na ongezeko la bei ya mafuta yaliyosafishwa kwenye soko la dunia, hususan Uarabuni yalipoagizwa. Bei hiyo katika soko la dunia imepanda kwa asilimia 6.3 kwa petroli na asilimia 2.2 kwa dizeli ikilinganishwa na mwezi uliopita.

Ongezeko jijini Dar es Salaam limechangiwa pia na mabadiliko ya gharama za uagizaji wa mafuta (premiums) zilizoongezeka kwa wastani wa asilimia 3.58 kwa petroli na asilimia 4.35 kwa dizeli, sambamba na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji, bima na faida za waagizaji.

Ikilinganishwa na mwezi Julai, Ewura imesema bei ya rejareja ya mafuta yaliyoingia kupitia Bandari ya Tanga imeongezeka kwa Sh19 kufikia Sh3,229 kwa petroli na Sh14 kufikia Sh3,138 kwa dizeli. 

Wakazi wa kusini mwa Tanzania wao ndiyo watatoboa zaidi mifuko ya baada ya bei ya petroli kwa lita kuongezeka kwa Sh92 kwa lita kutoka mwezi uliopita hadi Sh3,304, ikiwa ni ongezeko kubwa kurekodiwa ndani ya mwezi kati ya bei zote za bidhaa hizo zinazoanza kutumika leo.  

Katika bei hizo zilitolewa usiku wa kuamkia leo, bei ya rejareja ya dizeli imeongezeka kwa Sh16 hadi kuuzwa Sh3,140 kwa lita. 

Licha ya bei kuongezeka Tanga na Mtwara, gharama za uagizaji wa mafuta zimepungua kwa wastani wa asilimi 6.75 kwa petroli na dizeli katika Bandari ya Tanga; na pia zimepungua kwa wastani wa asilimia 7.54 kwa mafuta ya petroli na dizeli katika Bandari ya Mtwara kulinganisha na mwezi Julai.

Kuongezeka kwa bei ya mafuta hufanya watumiaji wa vyombo vya moto kutumia fedha nyingi zaidi kupata kiwango kile kile cha nishati jambo linalochochea kupanda kwa bei za huduma na bidhaa kutokana na kupaa kwa gharama za usafirishaji. 

Baadhi ya wamiliki wa vyombo binafsi vya usafiri jijini Dar es Salaam wameweza kuepuka makali ya gharama zinazobadilika badilika za dizeli na petroli kwa kubadilisha mifumo ya utumiaji wa nishati kwenye vyombo vyao kwa kuhamia kwenye gesi asilia (CNG).

Wakazi wa Kyerwa mkoani Kagera ndiyo watanunua petroli kwa bei ya juu zaidi nchini kwa mwezi Agosti ikiwa ni Sh238 zaidi ya kiwango wanachonunua wenzao wa Dar es Salaam. Bei ya petroli katika eneo hilo itauzwa Sh3,469.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV