Makali mgao wa umeme kupungua Desemba 2022

November 2, 2022 11:35 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya Serikali kukamilisha mradi wa Kinyerezi I.
  • Mradi huo utazalishaji megawati 185.
  • Kwa sasa kuna upungufu wa megawati 190 zinazochangia mgao wa umeme. 

Dar es Salaam. Serikali imesema makali ya mgao wa umeme nchini yanaweza kupungua mwezi ujao wa Novemba baada ya kukamilika kwa miradi ya umeme ukiwemo wa Kinyerezi I uliopo jijini Dar es Salaam. 

Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato ameliambia Bunge leo Novemba 2, 2022 jijini Dodoma kuwa mwezi ujao mradi wa Kinyelezi I utakamilika na kuingiza megawati 185 katika gridi ya Taifa.

Amesema megawati hizo zitapunguza makali ya mgawo wa umeme unaendelea hivi sasa katika maeneo mbalimbali nchini ambao umeibua mjadala mpana miongoni mwa Watanzania wakiwemo Wabunge.

Aidha, Serikali ina mpango wa kutenga Sh500 bilioni kwa ajili ya kusaidia ukarabati wa miundombinu chakavu, jambo likalkosaidia kuokoa umeme unaopotea na kuongeza ufanisi wa uzalishaji wa umeme nchini. 


Zinazohusiana:


Kwa nini mgao wa umeme?

“Tatizo tulilonalo ni upungufu katika vyanzo vya kuzalisha umeme, mheshimiwa Spika, kwa sasa tuna upungufu wa megawati 190 katika vyanzo vya kuzalisha umeme nchini,” amesema Byabato.

Byabato ametoa kauli hiyo baada ya Spika wa Bunge Dk Tulia Akson kumtaka kueleza kuhusu kukatika katika kwa umeme nchini, jambo ambalo limekuwa likileta usumbufu mkubwa kwa wananchi wakiwemo wafanyabiashara. 

Dk Tulia alimtaka Naibu Waziri huyo kutoa kauli ya Serikali baada ya Mbunge wa Ndanda (CCM), Cecil Mwambe kutaka kujua mkakati wa Serikali kumaliza kero ya kukatika kwa umeme mara kwa mara ikiwemo mikoa ya kusini.

Spika Tulia ameitaka Wizara ya Nishati, kulitazama upya suala la mgawo wa umeme kwa kutoa kipaumbele kwa baadhi ya maeneo ambayo yanahitaji umeme zaidi ikiwemo shughuli za viwanda na huduma muhimu ikiwemo afya.

 Amesema hiyo itasaidia kupunguza hasara wanayopata watu hasa wafanyabiashara katika maeneo yao. 

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW