Siyo kweli unatakiwa kutoa Sh800,000 kuunganishiwa umeme nyumbani

September 6, 2022 12:51 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Serikali yatoa ufafanuzi baada ya kuwepo mjadala mkali.
  • Yasema Serikali hutoa ruzuku ili kudia ghara za kuunganisha umeme majumbani.

Dar es Salaam. Wizara ya Nishati imesema gharama halisi ya kuunganisha huduma ya umeme katika nyumba kwa wakazi wa mijini na vijijini ni Sh800,000.

Hata hivyo, kiasi hicho hakitolewi na wananchi kama inavyodaiwa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii.

Serikali imekuwa ikitoa ruzuku ili kupunguza gharama hiyo ili kuwawezesha Watanzania kuipata kwa urahisi kuwawezesha kutekeleza shughuli za maendeleo. 

Waziri wa Nishati, January Makamba aliyekuwa akizungumza Septemba 5, 2022 katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV, alisema fedha hizo zingekuwa zinatolewa na wananchi zingesaidia  kuboreshea huduma zingine ikiwemo kupanua mtandao wa umeme.

“Mwananchi akitakiwa kulipa Sh 27,000 ajue Serikali inachangia Sh773,000 kutoka kwenye mfuko wake na tukisema mteja alipe Sh321,000 kwa kiwango hicho ajue Serikali inachangia Sh 489,000, ni muhimu lijulikane hili.

Amesema gharama halisi za umeme na kuunganishiwa ni bei ambazo zinawekwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) kwa hiyo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) haliwezi kutoza kiwango zaidi ya kilichopangwa na mamlaka husika.

Amesema Tanesco inaingia gharama za kununua waya, mita na nguzo ambazo hutumika kumuunganishia mteja umeme. 

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV

Sakata bei ya mafuta kupanda latua BoT, Naibu Gavana atoa ufafanuzi

Sakata bei ya mafuta kupanda latua BoT, Naibu Gavana atoa ufafanuzi

Nukta TV

BoT yabakiza Riba ya Benki Kuu 5.75% kudhibiti mfumuko wa bei

BoT yabakiza Riba ya Benki Kuu 5.75% kudhibiti mfumuko wa bei

Nukta TV