Majaliwa atoa maagizo mazito pikipiki za maafisa ugani

June 8, 2022 11:09 am · David
Share
Tweet
Copy Link
  • Aagiza pikipiki zilizopo wizarani wapewe maafisa hao.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku kwa Wizara ya Kilimo iwe imeondoa pikipiki zote katika ofisi za wizara hiyo zilizopo jijini Dodoma na kuzikabidhi kwa wakurugenzi wa halmashauri nchini.

Majaliwa aliyekuwa akikagua Ofisi za Wizara ya Kilimo zilizopo eneo la VETA, Dodoma na kukuta pikipiki zilizotolewa kwa ajili ya maafisa ugani zikiendelea kuwepo, amesema kuanzia leo Juni 8, 2022 hadi Juni 12, 2022 pikipiki hizo ziwe zimeondolewa kwa sababu zimekaa muda mrefu. 

“Hii haikubaliki, Wakurugenzi wote waandikiwe barua waje wazichukue, kama kuna ufungaji wa plate number utafanyika huko huko. Jumapili saa 10 jioni ziwe zimefika kwa wahusuka,” amesema Majaliwa.

Aprili 4, 2022, Rais Samia Suluhu Hassan alizindua ugawaji wa vitendea kazi vilivyoandaliwa na Wizara ya Kilimo kwa ajili ya maafisa ugani wote nchini. Vifaa ni pamoja na pikipiki.

Amesema tayari Rais Samia alishazikabidhi kwa ajili ya kupelekwa kwa maafisa ugani, hivyo kitendo cha pikipiki hizo kuendelea kubaki katika eneo hilo hakikubaliki.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Profesa Siza Tumbo amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba wamepokea maelezo hayo na watayafanyia kazi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
14 Oct, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

Nukta TV

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

Nukta TV

BoT yauza tani 5 za dhahabu kuongeza fedha za kigeni

BoT yauza tani 5 za dhahabu kuongeza fedha za kigeni

Nukta TV