Bodi ya mikopo yatenga Sh1.06 trilioni, makusanyo yapaa

October 14, 2026 1:31 pm · Method Allen
Share
Tweet
Copy Link
  • Imefanikiwa kukusanya Sh235.5 bilioni, ikiwa ni sawa na asilimia 107 ya lengo la Sh220 bilioni lililokuwa limewekwa apo awali.
  • Wanafunzi 300,000 wanatarajiwa kunufaika na ongezeko hilo.

Dar es Salaam. Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (HESLB) imetenga jumla ya Shilingi trilioni 1.06 kwa ajili ya mikopo na ruzuku za wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2026/2027.

Kwa mujibu wa HESLB, Hatua hiyo mpya inatarajia kuwanufaisha wanafunzi takribani 300,000, ikilinganishwa na Sh916.7 bilioni zilizotengwa mwaka 2025/2026 na kuwanufaisha wanafunzi 289,932.

Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 15.63 za fedha zilizotengwa kuwawezesha wanafunzi hao wa elimu ya juu.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dk Bill Kiwia,valiyekuwa akiwasilisha mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita alisema uwekezaji huo unaakisi dhamira ya Serikali ya kuhakikisha elimu ya juu inawafikia vijana wengi zaidi nchini.

“Bodi imepanua wigo wa ufadhili kwa kujumuisha wanafunzi wa masomo ya Stashahada ‘Diploma’ pamoja na mpango maalumu wa Samia Scholarship, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kujenga rasilimaliwatu yenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira na maendeleo ya nchi”. Amesema Dk Kiwia Oktoba 12, 2026 Jijini Dar es Salaam.

Katika kuthibitisha utekelezaji wa bajeti hiyo mpya, HESLB tayari imetoa Sh535.7 bilioni katika awamu ya kwanza ya upangaji wa mikopo.

Kiasi hicho kimewanufaisha  wanafunzi 165,775 wa mwaka wa kwanza na wale wanaoendelea na masomo. 

Katika hatua nyingine HESLB imesema wanafunzi 74,769 wa Shahada ya kwanza wamepangiwa kiasi cha Sh246.88 bilioni huku wanafunzi 8,538 wa Stashahada wakipangiwa kiasi cha Sh22.9 bilioni.

Wanafunzi wengine 873 wanao nufaika na programu ya Samia Skolashipu pia wametengewa Sh4.5 bilioni kwa ajili ya kugharamia elimu hiyo ya juu.

Bodi imepanua wigo wa ufadhili kwa kujumuisha wanafunzi wa masomo ya Stashahada ‘Diploma’ pamoja na mpango maalumu wa Samia Scholarship, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kujenga rasilimaliwatu yenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira na maendeleo ya nchi | Picha Canva

Kwa upande wa wanafunzi wanaoendelea na masomo, mchanganuo unaonyesha kuwa wanafunzi 79,115 wa shahada ya awali wamepangiwa Sh252.4 bilioni, huku wanafunzi 1,554 wa stashahada wakipangiwa Sh3.8 bilioni, na wanufaika 926 wa Samia Scholarship wakipangiwa ruzuku ya Sh5.1 bilioni. 

HESLB meeleza kuwa inaendelea kutoa awamu zinazofuata za mikopo pamoja na fedha ya kujikimu kadiri inavyopokea uthibitisho wa udahili kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na matokeo ya walioko chuoni, huku ikiwakumbusha waombaji wote kuendelea kufuatilia taarifa za maombi yao kupitia mfumo wa taarifa za wanafunzi (SIPA).

Makusanyo yavunja rekodi

Katika hatua nyingine, Bodi hiyo imerekodi kiwango cha juu zaidi cha urejeshaji wa mikopo tangu kuanzishwa kwake, ambapo katika mwaka wa fedha 2025/2026, Bodi imefanikiwa kukusanya Sh235.5 bilioni, ikiwa ni sawa na asilimia 107 ya lengo la Sh220 bilioni lililokuwa limewekwa apo awali.

Dk Kiwia alibainisha kuwa mafanikio hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na matumizi ya kampeni za hamasa na uelimishaji kama vile ‘Fichua’ na ‘KiduchuFreshTunasonga’, pamoja na kuweka mifumo rahisi inayowapa fursa wanufaika wenye kipato kidogo kuanza kurejesha kidogo kidogo kulingana na uwezo wao.

Pamoja na mafanikio hayo ya kiasi cha fedha na ongezeko la wanufaika, Mkurugenzi Mtendaji huyo alikiri kuwa bado kuna maeneo yanayohitaji maboresho ili kuifanya Bodi hiyo iwe endelevu zaidi.

“Pamoja na mafanikio haya, bado kuna maeneo yanayohitaji kuboreshwa, yakiwemo mfumo wa mawasiliano na wanufaika, uwasilishaji wa taarifa sahihi na kwa wakati, pamoja na kuongeza juhudi za kuwafikia wadaiwa waliosoma na walio katika sekta isiyo rasmi,” alisisitiza Dk. Kiwia.

Hata hivyo, bodi hiyo imeendelea kuimarisha mifumo yake ya kidijitali na mikakati ya ufuatiliaji ili kuhakikisha mfuko wa mikopo ya elimu ya juu unakuwa endelevu kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

Nukta TV

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

Nukta TV

BoT yauza tani 5 za dhahabu kuongeza fedha za kigeni

BoT yauza tani 5 za dhahabu kuongeza fedha za kigeni

Nukta TV